Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

POLISI IKWIRIRI YATANGAZA KUTOA MIL 20 KWA ATAKAETOA TAARIFA ZA MAJAMBAZI WALIOVAMIA KITUO CHA POLISI NA KUUA ASKARI 2 NA KUCHUKUA BUNDUKI 5 NA RISASI 60 USIKU WA KUAMKIA

tiko tiko

Askari wawili wameuawa katika kituo kidogo cha polisi cha IKWIRIRI mkoani PWANI usiku wa kuamkia leo na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. 

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi mkoa wa PWANI, ULRITCH MATEI amesema watuhumiwa wa uhalifu huo wanadaiwa kuiba bunduki 5, risasi 60 na silaha zinazotumika kupiga mabomu ya machozi mbili.

Kamanda MATEI amesema polisi inaendelea na msako mkali kuwatafuta wahalifu wa tukio hilo huku akiwaomba wakazi wa mikoa ya PWANI, LINDI, MTWARA, DSM, na visiwa vya ZANZIBAR kushirikiana na polisi kutoa taarifa za watu watakaowatilia shaka. 

Jeshi la polisi limeahidi kutoa zawadi ya shilingi MILIONI 20 kwa watakaofanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top