tiko
tiko
INATOSHA! Mrembo,
Happiness Wilfred Nassari (27), ameibuka na kudai kuwa amekuwa akisali
bila nguo kwenye ibada ya imani ya Freemason inayosifika kwa ushirikina.
Mrembo, Happiness Wilfred Nassari (27) anayedai kushiriki imani ya kifreemason.
Katika mahojiano yaliyofanyika hivi
karibuni ndani ya chumba cha habari, makao makuu ya gazeti hili Bamaga,
Mwenge jijini Dar, Happiness alisema kuwa, alianza kuingia kwenye imani
hiyo kwa kwa kupitia kaka yake mmoja (jina tunalo) ambaye ni tajiri wa
kupindukia kutokana na kuwa mshiriki wa Freemason.
“Nilipojiunga ilikuwa si kwa matakwa
yangu, kwani nilianza kwa kupata matatizo ya kuumwa magonjwa ya
ajabuajabu, ikiwemo kutokwa na wadudu usoni kiasi cha kunitoa vidonda,”
alisema mrembo huyo huku akionesha makovu ya vidonda hivyo.
“Hali ilipokuwa mbaya, ilibidi niende
kwa mganga mmoja wa kienyeji ambaye aliniambia nimetupiwa majini ya
kunuka ambayo yanabadilika harufu kila mara, lakini alitaka nimlipe
shilingi milioni 5 ili anitibie, nikashindwa, nikaondoka.
“Kuna wakati vile vidonda vilisababisha
nianze kufuatwa na nzi wengi hadi watu wengine wakawa wanadai kusikia
harufu, ndipo nikaenda kwenye Kanisa la Tanzania Assemblies of God
(TAG), Arusha kwa Mchungaji Olduvic kuombewa ndipo nzi wakatoweka na
harufu kupungua,” alisema.
Moja ya alama za imani ya kifreemason.
Alisema baadaye alijikuta akiwa muumini
mkubwa wa Freemason lakini si kwa hiari yake. Akaongeza kuwa, alipewa
uwezo wa kusafiri mbali ya Tanzania kwa usiku mmoja na kukutana na
wazungu ambao anaamini wana uwezo mkubwa wa mambo ya kiroho kuliko
walokole wa siku hizi.
“Hali hiyo ilifika mahali mpaka nikaanza
kushirikishwa ibada zao kwa kusali bila nguo. Tulikuwa tunakwenda
kwenye hekalu la ibada tukiwa tumevaa lakini tukifika ndani tunavua nguo
na kubaki kama tulivyozaliwa na kuanza kusali. Hekalu hilo lipo
hapahapa Dar es Salaam, lakini naomba nisiseme lilipo.
“Jambo kubwa ambalo nataka kulisema kwa
leo, si kwamba nimeachana nao, bado nipo. Ila nimejikuta nikiwa sina
amani kwa kuficha habari hizi.“Ninachojua hata hapa ninapozungumza na
nyinyi wanajua kila kitu, kwani wananifuatilia bado kwa sababu
walishanipa fedha kwa ajili ya mtaji wa biashara, lakini kusema ukweli
sina amani,” alisema Happiness na kuanza kulia.
Alimalizia kwa kuweka wazi kwamba, kwa
wale wanaotafuta utajiri kwa kupitia imani ya Freemason, anawashauri
kuachana na akili hiyo kwani utajiri wao unakuwa na masharti mengi
ikiwemo kuua ndugu wakiwemo wazazi.Mrembo huyo ataanza kusimulia hatua
kwa hatua ya namna alivyokutana na Freemason mpaka alipo sasa. Soma
gazeti hili wiki ijayo.
tiko
tiko
Post a Comment