tiko
tiko
Wakizungumza
wakiwa porini kujadili hatma ya usalama wa wafugaji hao wakiwemo
wanaume kwa wanawake kutoka wilaya za Kilosa na Mvomero wamesema
hawakuusika na mgogoro uliosababisha mauaji ya mkulima katika bonde la
mgongola na hivyo kuomba serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama
wawasaidie kwani hivi sasa wagonjwa wanalazimika kutibiwa majumbani
wanafunzi hawaendi shule kwa kuhofia madereva wa bodaboda.
Nao
baadhi ya wafugaji waliojeruhiwa na kuporwa fedha wameeleza jinsi
walivyovamiwa na kupigwa kisha kunyanganywa simu na fedha na hivi sasa
wanaugulia majumbani na wanashindwa kwenda hospitali kupata matibabu kwa
hofu ya kuvamiwa na madereva wa bodaboda huku baadhi ya wanafunzi
wafugaji wanaosoma chuo cha St Josefu Morogoro nao wameelezwa kurudi
majumbani.
Wakati
haya yakitokea jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limewafikisha
mahakamani madereva wa boda boda 11 waliobainika kuhusika na matukio ya
kuvamia wafugaji ambapo wamesomewa mashataka mawili ya kuvamia wafugaji
kwanyakati tofauti mbele ya hakimu mkazi Maua Hamduni ambapo washtakiwa
wamenyimwa dhamana kwa hofu ya usalama wao na kurudishwa rumande .
tiko
tiko
Post a Comment