tiko
tiko
UPEPO umegeuka!
Imani ya kwamba wanaume ndiyo wamekuwa wakiwapa kipondo wake zao
imegeuka, safari hii mwanamke aliyejulikana kwa jina la Naomi Peter
akimpa kipondo ‘hevi’ mumewe John Shila mchana kweupe!
Wawili hao wakazi wa Misheni, jijini Mwanza waliibua timbwili la aina
yake ambalo liliwavuta watu wengi chanzo kikiwa ni mwanaume huyo
kumkataa mtoto aliyezaa na mwanamke huyo.
Akizungumza na waandishi wetu, mmoja wa mashuhuda alisema wawili hao
walioana na kuishi kama mke na mume na baadaye kupata mtoto mmoja wa
kike, baada ya miaka miwili ulitokea ugomvi na kusababisha mwanamke
kuondoka na ndipo John alipotumia mwanya huo kuoa mwanamke mwingine.
“Siku ya tukio, Naomi alimpeleka mtoto wake nyumbani kwa mzazi mwenzake
kutokana na kutopewa hela ya matumizi, wakati huo Shila alikuwa na
mwanamke wake mpya ndani, baada ya mabishano ya muda ndipo Naomi akaanza
kumshughulikia Shila kwa kumtandika mangumi.
“Jamaa alikuwa hapeleki matumizi kwa mzazi mwenzie, mbaya zaidi alikataa
na kudai mtoto si wake ndipo timbwili lilipoanzia,’’ kilisema chanzo
hicho.
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, wakati ugomvi huo ukiendelea
mwanamke wa John wa sasa alikuwa kimya ndani na kushuhudia mpenzi wake
akipokea kichapo kisha kumkabidhi mwanaye amlee na yeye akaondoka zake.
Hadi shuhuda wa habari hizi anaondoka eneo la tukio, muafaka juu ya kilichofikiwa ulikuwa bado haujapatikana.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment