tiko
tiko

Na hivi vya muda mfupi nitahakikisha kuwa lazima nivitekeleze ile wiki
ya kwanza tu ya kukabidhiwa rungu. Niwe mkweli kipaumbele cha kwanza
kitakuwa ni kumshughulikia mama mwenye nyumba wangu. Unajua huyu mama
ananinyanyasa sana kwa kashfa zake ambazo zinanifanya niwe namuogopa
nikimuona nanywea kama kuku kanyeshewa mvua.
Kila tukipishana ananikumbusha jinsi nilivyo maskini wa kutupwa nisiye
na mbele wala nyuma, eti ndiyo maana napanga kwake na hata kodi
inanishinda. Kwa hiyo ile nikitangazwa tu kuwa nimechaguliwa, huyu mama
nitamuweka ndani kwa kosa la kutukana kiongozi wa ngazi za juu.
Hicho ndicho kipaumbele changu cha kwanza, pia nitapita dukani kwa Mangi
kumtangazia kuwa kama alikuwa ananidai deni limefutika, habari ndiyo
hiyo. Lazima nitafute suti kali na kuanza kupitia vijiwe vya washkaji
wote niwape taarifa kuwa kuanzia sasa lazima waniamkie shikamoo,
ukiwaachia hawa wanaweza kujiona eti wao nao taip yako!
Sasa naona ni muhimu hapa nitoe ushauri kwa yeyote atakayechaguliwa
wadhifa kama huu ni vitu gani muhimu kufuata. Kwanza ni kuwahi kufanya
mambo yetu yale ya Kiafrika, bila utamaduni, utaadhirika mapema sana,
hivyo ni muhimu kutengeneza kinga kuzuia watu wenye roho mbaya.
Hapa inahitajika kupata mganga mzuri, mnaweza kunitafuta niwaunganishe
kwa babu yangu, maana babu ni kiboko. Kwanza babu atakuchemsha kwenye
chungu kimoja kikubwa hii ni kusafisha nyota, ukiwa na nyota safi
unakuwa na uwezekano wa kupanda cheo harakaharaka, baada ya hapo
atakuchanja chale ili wabaya wakituma makombora yasikupate tena
yawarudie, si unajua mswahili alivyo, asikuone umepata ataanza kutafuta
kila njia ukikose.
Baada ya hapo utapata dawa za kukufanya watu wakusikilize, unajua bila
hizi dawa ukiwa unatoa amri utakuta watu hawajali sasa hapo unakuwa
mkubwa feki, hii mara nyingi inakuwa hirizi ya kuvaa shingoni. Kisha
babu atakupa hirizi za kuhakikisha huondolewi kwenye cheo chako, hirizi
hizi utaziweka sehemu kadhaa, moja unavaa mkononi, nyingine unaiweka
kwenye kiti ofisini kwako, jingine kwenye gari, nyingine utafukia kwenye
geti la nyumba mpya utakayopewa.
Kisha utakuwa na hirizi ya kuvaa kiunoni, hii ni muhimu ili kukiwa na
vikao vya kamati mbalimbali watu wote wanakusikiliza wewe tu. Ni muhimu
kuwa na hirizi nyingine ya kutembea nayo kwenye pochi kulinda pesa
unazopata zisichukuliwe na chuma ulete, ukajikuta mshahara unapata
lakini haukai.
Kikubwa ni muhimu kuhakikisha unarudi kwa Babu kila baada ya mwezi
kufanya maboresho ya hizi kinga, maana lazima ujue maadui wakikujaribu
wakiona wamekwama wanaenda kuongeza ufundi hivyo muhimu kuboresha kinga
hizi.Nategemea kupata simu kwa wingi kwa wahusika ili kuweza kuboresha
ulinzi huu shirikishi!
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment