tiko
tiko
Kwa zaidi ya siku tatu mtu wako wa nguvu nimekuwepo hapa Barcelona Hispania
kuhudhuria maonyesho ya kiteknolojia duniani ambapo makampuni
mbalimbali na makubwa ya dunia yamekusanyika kuonyesha ukali wao kwenye
maswala ya digital.Mpaka sasa HUAWEI wameendelea kuongoza kwa kuzimiliki headlines kubwa za dunia kutokana na bidhaa mbalimbali walizozindua ambapo leo ilikua ni zamu ya hii saa ya kisasa.
Ni saa ambayo pamoja na mambo mengine, inakupa muda kama zilivyosaa nyingine, simu yako inaweza kuwa mbali na wewe lakini hii saa ikakuonyesha nani anakupigia, inakupa utabiri wa hali ya hewa, kuna sehemu ya kukutunzia kumbukumbu za vitu unavyotaka kufanya.
Kingine kikubwa nilichopenda ni kwamba ina uwezo wa kukutelea taarifa mpya kila wakati kama umepata msg Facebook, kwenye email na mitandao mingine ya kijamii.
Hizo ni baadhi ya sifa zake tu.
n
Unaweza kutazama video ya maelezo mengine ya hii saa kwa kubonyeza hapa chini na ukishamaliza kuitazama usisahau kuacha comment yako manake hujui ni zawadi gani inaweza kukuangukia, vilevile kwenye facebook ya millardayo ataekuwa wa elfu moja kubonyeza like ya post ya video kuhusu hii saa nitamzawadia saa hii ikishaanza kuuzwa madukani.
tiko
tiko
Post a Comment