tiko
tiko
Kutoa siri za taifa kubwa kama Marekani
ni kesi kubwa sana, iwapo wakikukamata watu wa usalama wa nchi hiyo na
ukafikishwa Mahamakani ni ishu kubwa ambayo hata Edward Snowden inamtia hofu.
Snowden
alikuwa mmoja ya wafanyakazi wa CIA, baadaye aliendelea kazi sehemu
nyingine ikiwemo Kampuni ya Dell kutokana na utaalamu wake kwenye
masuala ya computer, jina lake liliingia kwenye headlines kubwa duniani
baada ya kuvujisha taarifa za siri za ndani za taifa la Marekani,
ikiwemo ishu ya watu wa usalama wa nchi hiyo kuchunguza simu mbalimbali
pamoja na za viongozi wa mataifa mengine duniani.
Mwanasheria wa Edward Snowden
amesema jamaa huyo yuko tayari kabisa kurudi Marekani lakini atarudi
kama watamhakikishia haki kutendeka wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake.
Mwanasheria huyo Anatoly Kucherena amesema Snowden
ana hamu kubwa kurudi nyumbani kwao Marekani lakini hofu yake kubwa ni
jinsi ambavyo atapokelewa japo Mwanasheria Mkuu wa Marekani kamuahidi
kwamba hatohukumiwa kifungo cha maisha.
Snowden
bado anaweza kusafiri kwenda sehemu nyingine yoyote duniani kutokana na
kwamba ana hati ya kuishi Russia kwa miaka 3 na amekuwa ndani ya nchi
hiyo kwa kipindi chote ambacho amekuwa akitafutwa na Marekani baada ya
kuvujisha siri hizo.
Wenzetu huwa hawakawizi mambo, unaambiwa huu utata wa maisha ya Snowden
tayari wameingia location wanaandaa filamu ya maisha yake muda wowote
ikitoka huenda tukamfahamu zaidi jamaa huyo kupitia movie hiyo ambayo
actor Joseph Gordon-Levitt ndio star ambaye amecheza kama Snowden.
Nitaendelea kukupatia kila stori
inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia
Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment