tiko
tiko
Siri imefichuka! Bwa’mdogo a.k.a Serengeti Boy kutoka Kundi la
Makomando, Fredy Felix amesimulia namna alivyofaidi penzi la staa wa
Bongo Movies, Jacqueline Walper Massawe ‘Wolper’.
Akizungumza na GlobalTV Online kwenye mahojiano maalum juzikati, dogo
huyo alisema kuwa katika maisha yake ya kimapenzi hakuna mwanamke ambaye
aliwahi kutoka naye na kujiachia kwa furaha kama ilivyo kwa Wolper.
“Kiukweli msichana pekee ambaye nimewahi kuwa naye katika mapenzi na
kumpenda kwa dhati ni Wolper pekee.“Mara yangu ya kwanza kukutana naye
ilikuwa kama ‘sapraiz’ vile (habari zinasema kwamba walikutana maeneo ya
Kinondoni), alipoingia kwangu nashukuru naye alinipenda na kunifanyia
kila nilichohitaji.
“Nampenda sana Wolper na kila siku nimekuwa nikiahidi kwamba huyo ndiye
mwanamke pekee ambaye nitakuja kuishi naye hata kama ni uzeeni maana
ninampenda kutoka moyoni.“Sidhani kama moyo wangu utampenda mwanamke
mwingine kama nilivyompenda Wolper. Kiukweli niliinjoi sana penzi lake,”
alisema Fredy huku akijutia kumwagana naye bila sababu ya msingi.
Alipotafutwa Wolper ili kupata undani wa ishu hiyo simu yake ilipokelewa
na aliposomewa mashtaka yake alikaa kimya bila kujibu chochote. Hata
hivyo jitihada za kumtafuta zinaendelea.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment