tiko
tiko
Haikuwa kitu cha kawaida wakati gari
hilo kubwa likishusha mfuniko huo wa zege kwenye kaburi la mwimbaji huyo
maarufu wa nyimbo za uhamasishaji za CCM na kiongozi wa kundi la
Tanzania One Theatre (TOT), lakini majonzi yaliwafanya waombolezaji
kulichukulia tukio hilo kuwa la kawaida.
Safari ya Komba, iliyoanza miaka 61
iliyopita kwenye kijiji cha Lituhi ambako aliazikwa jana, ilikamilishwa
kwa salamu mbalimbali ambazo zilielezea ushupavu wa kapteni huyo mstaafu
wa jeshi.
Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya
wananchi, wakiwamo viongozi mbalimbaliwakiongozwa na Rais Jakaya
Kikwete na mkewe Salma, yalifanyika katika makaburi ya Misheni,katika
Kijiji cha Lituhi (Bundi) wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Nyuso za majonzi zilitawala kwa
waombolezaji waliojitokeza nyumbani kwa marehemu, takriban mita 500
kutoka katika makaburi hayo na baadaye katika misa iliyofanyika kwenye
uwanja wa Shule ya Msingi ya Lituhi, ikiongozwa na Askofu John Ndimbo wa
Jimbo Katoliki la Mbinga.
Kaimu katibu wa Bunge, John Joel,
akisoma wasifu wa marehemu, alisema Kapteni Komba aliyefariki dunia
Februari 28, mwaka huu akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya TMJ jijini
Dar es Salaam, alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na
mara kadhaa Ofisi ya Bunge ilimpeleka India kwa matibabu. Pia alikuwa na
tatizo la kisukari ambalo ndilo lililochukua maisha yake.
Mazishi hayo yalishuhudiwa na viongozi
mbalimbali, akiwamo Edward Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu, Waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Utaratibu na Bunge), Jenister Mhagama na mbunge wa
Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi.
Wengine ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani
Kikwete, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Ali Abdallah Ali, Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya na Spika
wa Bunge, Anne Makinda.
Uwanja wa ndege
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea,
viongozi mbalimbali waliwasili kwa ndege za kukodi na Lowassa ndiye
aliyefungua mlango kwa ndege iliyotua saa 2:33 asubuhi akiambatana na
mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani.
Haikupita muda mrefu, ndege nyingine
ilitua saa 2:50 ikiwa na Spika Makinda na msafara wake uliomjumuisha
mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe.
Saa 3:22 ilitua ndege iliyobeba ujumbe
wa CCM ukiongozwa na Kinana. Wengine waliokuwamo ni naibu katibu mkuu
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, katibu wa itikadi
na uenezi, Nape Nnauye na mwimbaji wa kikundi cha TOT, Khadija Kopa. Pia
baadaye Rais Kikwete alitua na ndege ya Serikali.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment