Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Ndoa ya Babu na Bibi nayo iko kwenye HEADLINES

tiko tiko

wazeeTumezoea kuona vijana au watu wa makamo kufunga ndoa lakini ilikuwa ajabu kwa vikongwe hawa kuchukua uamuzi huo wakiwa na umri mkubwa.
Vikongwe hao Dikam mwenye umri wa miaka 107 na Ka’a Nafung mwenye miaka 95 Nigeria wameamua kufunga ndoa huku wakiwashangaza watu kwa uamuzi wao huo kutokanana umri wao.
Imeelezwa kuwa ndoa hiyo ilifungwa kutokana na kila mmoja mwenza wake kufariki dunia na kuwaacha wapekwe hivyo kuamua kutafuta faraja na kukutana kisha kuamua kufunga ndoa.
wazee
Dikam na Ka’a Nafung wakiwa na nyuso za furaha siku ya harusi yao
Bibi harusi ana mtoto mwenye umri wa miaka 65 ambaye ndiye pekee aliyebakia baada ya wengine kufariki.
Ndoa hiyo ilifungwa katika kanisa la Christ in Nations (COCIN) ambapo watu wengi walifurika kushuhudia ndoa hiyo huku wakiwapongeza kwa hatua hiyo.
Akisimulia historia ya maisha yake bwana harusi amesema alikuwa na wake saba na watoto 32 enzi za ujana wake, wakati huo alikuwa hamtambui Mungu na alikuwa na maisha ya kuoa na kuacha kila wakati.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top