tiko
tiko
Ni zaidi ya mwezi mmoja Bobbi Kristina, mtoto wa marehemu mwanamuziki Whitney Houston
amelazwa Hospitali baada ya kukutwa akiwa hana fahamu ndani ya bafu
nyumbani kwake Georgia, Marekani ambapo tukio hilo linahusishwa na
utumiaji wa dawa za kulevya.
Bado kumekuwa na ripoti za kuvutana
kuhusu hali yake kiafya, wapo wanaosema hali ni mbaya sana lakini
familia yake mara nyingi imekanusha kuhusu taarifa hizo.
Jana ilikuwa birthday yake kutimiza
miaka 22, ndugu wametuma salamu zao kumtakia heri ya kuzaliwa huku
wakionesha matumaini yao hali ya kiafya ya Bobbi kuendelea vizuri; “leo ni sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, anatimiza miaka 22.. tunaomba muendelee kumkumbuka kwenye maombi ili apone..“
Happy Birthday baby I wish I was there with you to hold you and be by your side
— Nick Gordon (@nickdgordon) March 4, 2015
Hiyo ni tweet aliyoandika Nick Gordon akituma salamu za birthday kwa mpenzi wake, Bobbi Kristina.tiko
tiko
Post a Comment