tiko
tiko
Waziri
wa Ujenzi, Dk John Magufuli jana aliungana na viongozi wenzake wa
Serikali kuwamwagia sifa viongozi wa vyama vya upinzani baada ya
kumwelezea Mbunge wa Hai na Mwenyekiti Chadema, Freeman Mbowe kuwa ni
mpigania maendeleo ya wananchi na kwamba alitakiwa awe malaika.
Dk Magufuli alimuelezea kiongozi huyo wa
upinzani bungeni kuwa ni mtu ambaye anafuatilia maendeleo ya watu bila
ya kujali itikadi zao.
Waziri huyo ameungana na Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kusifu utendaji wa viongozi wa upinzani.
Februari 10, Rais Kikwete alisifu
utendaji wa meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael wa kuwaletea
maendeleo wananchi, na siku 12 baadaye Waziri Pinda alimsifu mbunge wa
Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kwa kuwa kiongozi wa
kwanza kuchangia vitanda 30 kwenye Hospitali ya Frelimo.
Jana, Dk Magufuli alimmwagia Mbowe sifa
hizo katika mkutano wa hadhara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya
Kwasadala-Masama-Machame katika Jimbo la Hai inayojengwa kwa kiwango cha
lami.
“(Mbowe)Unadhihirisha kwamba maendeleo
hayana chama na kwa kweli tukienda hivi Tanzania itakuwa ni nchi ya
kutolewa mfano. Sincerely (kwa dhati) nakupongeza Mbowe na Mungu
akubariki,” alisema.
Kabla ya Dk Magufuli kutoa pongezi hizo,
Mbowe aliwataka wanasiasa kutekeleza ahadi zao kwa vitendo kwa kuwa
maendeleo hayana itikadi.
“Mimi naamini maendeleo hayana itikadi.
Jambo jema likifanywa na chama chochote cha siasa ama kiongozi wa chama
chochote au Mtanzania, kama ni jema anastahili kupongezwa,” alisema
Mbowe.
“Hakuna aibu ya kukiri pale jambo jema
linapofanyika. Ujenzi wa Barabara ya Kwasadala-Mula-Machame ni jambo
jema,” alisisitiza Mbowe.
Hata hivyo, alitumia mkutano huo wa
hadhara uliofanyika Kijiji cha Masama kumuomba Dk Magufuli atoe maagizo
ya kiserikali baada ya viongozi wawili wa CCM kutishia kuchoma moto
greda lake.
“Nimenunua greda ili tusaidiane na
Serikali, lakini juzi diwani na mwenyekiti wa kijiji walitishia kuchoma
moto greda eti kwa sababu mbunge hajapewa kibali cha kuchimba barabara,”
alilalamika.
Mbowe alisema vyama vya siasa ni lazima vifanye pamoja kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment