tiko
tiko
Mara
nyingi mtu akisumbuliwa na panya nyumbani kwake hufuga paka ili kuweza
kutokomeza panya lakini kuna mwingine anawapenda na kuamua kufuga hata
kama lengo lake sio hilo.
Huko Japan katika kisiwa cha Aoshima
ulifanyika mpango wa kufuga paka kwa lengo la kutokomeza panya lakini
baadaye paka hao wamegeuka kuwa kivutio kikubwa cha utalii katika kisiwa
hicho ambacho watu wanaoishi hapo ni 22 pekee lakini kimezingirwa na
paka.
Paka
hao waliletwa wachache kuangamiza panya ambao walikuwa wakiharibu
mitumbwi lakini kwa sasa paka wamezaliana na idadi yao kufikia zaidi ya
120.
Paka
hao wanaishi kwa kula chakula mtaani na mabaki ya chakula yanayotupwa
kwenye majalala, kisiwa hicho ambacho hakina maduka wala Hoteli kwa sasa
kinajulikana kama ‘Cat Island’, paka wao kwa sasa wamekuwa kivutio cha utalii kwa wageni wanaotembelea.
Unaweza kutazama video kwa kubonyeza playa hapa mtu wangu.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment