tiko
tiko
Staa wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego hivi karibuni aliweka wazi majibu yake baada ya kupima UKIMWI kupitia account yake ya Instagram na kwamba alikuwa yupo safi yaani(Negative).
Alipoulizwa sababu ya kupima ngoma alisema kuwa alikuwa akiumwa ugonjwa
wa Malaria na alikuwa hajaugua kwa muda mrefu na alipokwenda hospitali
ilibidi apime na ngoma ingawa ni kawaida yake kupima mara kwa mara.
‘’Nilipima baada ya kuumwa Malaria lakini huwa ni kawaida ya kupima
ngoma hata mke wangu(Siwema) alipokuwa mjamzito tulikwenda pamoja kupima
hospitali,"alisema Nay.
Alipoulizwa kama tangu alipoanza uhusiano na mke wake Siwema alishawahi kuchepuka alisema kuwa ni kweli alishawahi kufanya hivyo ila hawezi kusema ni mara ngapi ili kunusuru ‘ndoa’ yake.
Alipoulizwa kama tangu alipoanza uhusiano na mke wake Siwema alishawahi kuchepuka alisema kuwa ni kweli alishawahi kufanya hivyo ila hawezi kusema ni mara ngapi ili kunusuru ‘ndoa’ yake.
"Unajua ni mambo ya ujana, ni kweli nilishawahi kuchepuka lakini
siwezi kusema ni mara ngapi si unajua mama watoto anaweza kukasirika?
Lakini nilikuwa makini sana na namwomba sana msamaha mke wangu na
sitegemei kuchepuka tena,’’alisema Nay.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment