tiko
tiko
Mvua hiyo ya aina yake ilisababisha
nyumba 160 kuanguka na nyingine kuezuliwa paa kutokana na upepo mkali na
watu wengine 900 wameripotiwa kukosa makazi.
Watu wengi walifariki kutokana na
kuangukiwa na kuta za udongo za nyumba za wanakijiji hao na wengine
kuuawa kutokana na kuangukiwa na mawe makubwa ya barafu wakati
walipokuwa wakijaribu kutafuta hifadhi baada ya mapaa kutobolewa.
Mashuhuda wa tukio hilo waliliambia
gazeti hili kuwa mawe makubwa ya barafu yalikuwa yakidondoka usiku na
kuvunja nyumba za wakazi wa kijiji hicho ambazo nyingi ni za udongo.
Waokoaji walilazimika kufumua mabati
yaliyoanguka na kufukua vifusi kwa ajili ya kutoa miili ya watu
waliofariki na kuokoa walionusurika na baadaye kuwapakia kwenye malori
ili kuwapeleka hospitalini.
“Mimi tangu nianze uongozi wa umma sijawahi kukutana na tukio la aina hii,” alisema Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya.
“Nashindwa kulizungumzia (suala hili).
Hili ni tukio kubwa ambalo limepoteza uhai wa maisha ya watu hivyo
nashindwa nianzie wapi lakini kifupi wananchi wa Mwakata wamekumbwa na
msiba mzito,” alisema Mpesya, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya
Usalama ya Wilaya.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Ezekiel
Sanane alisema wakati mvua hiyo inanyesha ilikuwa na upepo mkali na mawe
makubwa ambayo yalikuwa yakitoboa nyumba na kutumbukia ndani na kuponda
watu, hali ambayo iliwafanya wengine kukimbilia nje ambako pia
walipigwa na mawe ya barafu na kufariki.
Sanane alisema wapo wengine walifunikwa kabisa na ukuta wa nyumba na kufariki, lakini wengine wamekufa wakiwa nje ya nyumba zao.
Hata hivyo mkazi wa kijiji hicho,
Paulina Nyalulu alisema alinusurika kifo baada ya kukimbilia barabarani.
Alisema baada ya kuona nyumba imejaa maji, yeye na familia yake
walikimbilia barabarani ambako walishuhudia nyumba zao zikianguka,
ingawa hakuna mtu aliyekufa.
“Tunamshukuru Mungu hakuna aliyekufa
kwenye familia hii lakini kama unavyoona vitu vyote, vikiwemo vyombo
pamoja na vyakula vimezolewa vyote maana maji yalijaa nyumba yote na
sisi tulikimbia na ndiyo ilikuwa usalama wetu,” alisema Nyalulu.
Taarifa za awali zilizotolewa na kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Jastus Kamugisha zilieleza kuwa idadi
hiyo inaweza kuongezeka kutokana na kazi ya kufukua miili kutoka kwenye
vifusi vya nyumba kuendelea hadi jana mchana
.
.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment