Takribani
miaka kumi na mbili sasa katika ndoa yetu na tumefanikiwa kupata watoto
wawili wote wa kiume. Mke wangu ana rafiki yake wa muda mrefu sana
(mchepuko wangu) tangu wakiishi udogoni na kusoma wote huko shinyanga
ingawa wametofautiana miaka kama minne hivi (huyo rafiki ndio mkubwa kwa
wife ila mdogo kwangu). Siku
ya jumatatu hii iliyopita (18-08-2014) baada ya kupata chakula cha
jioni na watoto kwenda kulala ndipo akanijia na hiyo "surprise" ambayo
sitasahau maishani mwangu. Aliniambia kama ninaweza nimuoe tu huyo
rafiki yake maana ana miaka takriban 34 sasa, na ni "bila bila"(kakosa
mume). Kwa kuwa sisi watu wa mkoa wa Mara kimila tunaruhusiwa ata
wake wanne, hivyo kumuweka ndani itakuwa nimempunguzia aibu ya kukosa
mume huyo mwanamke waliyeshibana sana, sasa machale yamenicheza, naona
kama wife ameshtukia "issue ya kuchepuka" sasa kanitega aniingize kingi. Najiuliza sijui ni mpe jibu gani wife aisee, naombeni busara wakuu wenzangu maanake naona kama "nimekamatika vile" |
Post a Comment