Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Shinyanga Yaendelea Kulia na Ukosefu wa Maji.....Hizi ni Picha za Wakazi wake wakiteseka kutafuta Maji

tiko tiko

WAKAZI wa manispaa ya Shinyanga na viunga vyake, wameendelea kuteseka kwa kukosa maji safi na salama kwa mfululizo wa siku nne sasa, baada ya mitambo ya kusukuma maji kutoka chanzo cha ziwa Victoria (Ihelele), na kusambaza maji hayo katika miji ya Kahama na Shinynga kupata hitilafu kwenye mfumo wa umeme.
  
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamezitupia lawama mamlaka za kusambaza maji hayo za mji wa kahama na Shinyanga (KASHUWASA) na ile maji safi na maji taka ya mji wa Shinynga (SHUWASA) kwa kushindwa kutatua tatizo hilo la maji mapema na kuwaacha wateja wao wakiendelea kutaabika kwa kukosa huduma hiyo muhimu.
  
Wakizungumza kwa niaba ya wenzao Naomi Masalu na Emmanuel Mabula, wamesema tatizo hilo la ukosefu wa maji limekuwa kero kwao, hali ambayo imekuwa ikikwamisha shughuli zingine za maendeleo na kupoteza muda mwingi wa kutafuta maji pembezoni mwa mji, kwenye visima vya maji ambavyo havina usalama.
  
Wamesema iwapo hali hiyo haitashughulikiwa mapema na  kuna hatari kubwa ya wakazi wa mji wa shinynga kuambukizwa magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu na kuharisha damu.
  

Naye mkurugenzi wa SHUWASA, Silivester Mahole, ambaye mamlaka yake inasambaza maji kwa wakazi wa mji humo, amesema tatizo hilo la ukosefu wa maji limetokana na upande wa KASHUWASA ambao mitambo yao imeharibika na kushindwa kusukuma maji.
  
Amesema baada ya kupata taarifa hizo za kuharibika kwa mitambo ya kuzalishia maji kutoka kwa wenzao (Kashwasa), wameamua kutumia vyanzo vyake vya zamani vya bwawa la Ning’wa na visima vidogo kusambaza maji mjini humo, ambayo nayo hayakidhi mahitaji ya wakazi hao.
  

Aidha kwa upande wake mkurugenzi wa KASHUWASA Clement Kivegaro, amekiri kuwepo kwa tatizo kwenye mitambo hiyo ya kuzalisha maji, ambayo imetokana na hitilafu ya umeme na kuwa mafundi wao wako kwenye matengenezo huku wakishirikiana na Shirika la umeme Tanesco, kwa ajiri ya kupata ufumbuzi wake ili wananchi waendelee kupata huduma hiyo kama kawaida.

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII

tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top