tiko
tiko
Christian
Bella (kulia) akijibu baadhi ya maswali ya wanahabari (hawapo pichani)
kuhusu maandalizi ya shoo yake ya Valentine kwenye Ukumbi wa Dar Live.
Christian
Bella (kulia) akiwapa vionjo vya wimbo wake mpya wa 'NASHINDWA'
wanahabari (hawapo pichani). Kushoto ni mmoja wa viongozi wa Malaika
Band, X-Bass Babu Bomba.
X-Bass Babu Bomba na Bella wakiwa katika picha ya pamoja na Mhariri Mwandamizi wa GPL, Walusanga Ndaki.
PREZIDAA wa Bendi ya Malaika, Christian Bella 'King of the Best
Melodies' amewaahidi shoo kali mashabiki wake watakaohudhuria katika
Ukumbi wa Kisasa wa Dar Live Jumamosi ijayo ambayo ni Siku ya
Wapendanao 'Valentine Day'.
Staa huyo ameyasema hayo hivi punde wakati wa mkutano na wanahabari wa
vyombo mbalimbali uliofanyika katika ofisi za Global Publishers.
Bella amesema atakuwepo ukumbini hapo mapema kuanzia saa 7 mchana na
atapiga picha za red carpet na mashabiki wake watakaohudhuria ukumbini
hapo.
Mbali na kuwahi ukumbini, Bella amewaandalia zawadi ya wimbo mpya uitwao
NASHINDWA ambao atauchia kwa mara ya kwanza ukumbini hapo na video yake
atakwenda kuifanyia nchini Afrika Kusini wiki ijayo.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment