tiko
tiko
Wasichana
22 walioingizwa nchini na mmiliki wa Continental Night Club , Omprakash
Singh kwa ajili ya kufanya biashara ya ukahaba wamerudishwa kwao Nepal
na India walikotoka.
Kamishna
wa Uhamiaji Udhibiti na Usimamizi wa Mipaka, Abdallah Abdullah, alisema
wasichana hao waliondoka jana baada ya kumaliza matibabu waliyokuwa
wakipata. “Wasichana waliokuwa wanaugua TB na UTI wote wamepona, tiketi
zilichelewa kidogo lakini imepatikana,”alisema.
Alisema
Singh ameshalipa faini ya Sh milioni 15 alizoamuliwa kulipa na
mahakama, pamoja na kulipa mishahara ya wasichana hao Dola za Marekani
30,625. Tangu wasichana hao walipobainika walikokuwa wamefichwa, Idara
ya Uhamiaji imekuwa ikiwasimamia kwa kuwapa matibabu na kufanikisha
safari ya kurudi nchini mwao.
Unadhani nini kinasabisha wamiliki wa sehemu za burudani kuagiza makahaba kutoka India?
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment