tiko
tiko
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Wazee
nchini wametishia kususa kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi
katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu nchini, iwapo
serikali haitatunga sheria ya kutetea haki zao.
Tamko
hilo lilitolewa jana mjini hapa na Mwenyekiti wao na Mtandao wa
shirika lisilo la Kiserikali la Mtandao wa Kinga Jamii (TSPN),
Theresa Minja, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.
Theresia
alisema kuwa mwaka huu kuna kuipigia kura Katiba Pendekezwa na uchaguzi
huo wa madiwani, wabunge na rais na kwamba wazee hawatakuwa tayari
kushiriki kama hawatapatiwa haki yao ya kisheria wanayoidai kwa kwa
serikali kwa miaka mingi sasa.
Alisema
ni miaka mingi tangu Sera ya Wazee ya mwaka 2003 kuhusu kupatiwa
matibabu bure kwa kundi hilo kutambuliwa katika maamuzi ya kijamii,
lakini imekuwa haitekelezeki kwa sababu hakuna sheria iliyotungwa.
“Inaoneka
kundi hili la Wazee hatuna umuhimu katika nchi hii na ndiyo maana
serikali haioni umuhimu wa kutusaidia kutunga sheria ambayo
itakayotupatia haki zetu za kimsingi ikiwa ni pamoja na kulipwa
pensheni hivyo hatuoni umuhimu wa kwenda kupiga kura maana
hatutambuliki, ” alisisitiza.
Alisema
wamekuwa wakiahidiwa kuwa mswada utawasilishwa bungeni kujadiliwa na
hatimaye kutungiwa sheria lakini tangu uwepo wa sera ya Wazee ya mwaka
2003, hakuna utekelezaji .
Theresia
alisema wamekuwa wakikutana na viongozi mbalimbali na kuwaomba
kulishughulikia serikali, lakini wamekuwa wakisikia kwenye matamko
ambayo hayana nguvu kisheria.
Katibu
wa Mtandao huo, Isiaka Msigwa, alisema serikali imeshughulikia baadhi
ya makundi nchini kwa kutungiwa sheria na kuwapuuza wazee.
Alisema
wazee hao kutoka mikoa ya Kagera, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dodoma,
Mbeya, Lindi, Ruvuma na Morogoro walikuwa mjini Dodoma kuonana na
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwalisisha kilio chao na wenzao.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment