tiko
tiko
Mashabiki
wa soka Misri huenda safari hii wakasahau kwa muda ligi kuu ya nchini
kwao baada ya Serikali kutangaza kuisimamisha ligi hiyo kwa muda
usiojulikana baada ya kuzuka vurugu zilizotokea jana na kusababisha watu
zaidi ya 20 kufariki.
Wengi wa waliofariki ni mashabiki wa timu ya Zamalek ambao
walifariki kutokana na msongamano mkubwa wa watu waliokuwa wakijaru
kuingia kwa nguvu uwanjani ambapo Polisi waliwafyatua mabomu ya machozi
wakati timu hiyo ilipokuwa ikipambana na timu ya ENPPI.
Taarifa ya Wizara ya mambo ya ndani ya Misri inasema kuwa Mashabiki wa Zamalek
walikuwa wanataka kuingia uwanjani kwa nguvu bila tiketi, Polisi
walijikuta wakitumia nguvu ya ziada kuwazuia ili wasifanye
uharibifu uwanjani.
Tukio hili limetokea ikiwa ni miaka
mitatu tangu itokee ishu kama hiyo ambapo wapenzi wa soka zaidi ya 70
walifariki wakati vurugu zilizotokea katika uwanja wa ndege wa Port Said.
Nitaendelea kukupatia kila stori
inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia
Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment