tiko
tiko
UZOEFU katika
maisha ni jambo zuri sana kwa sababu unakusaidia kwa mambo mengi, hasa
unapojikuta katika nyakati ngumu. Mara nyingi unapojikuta ndani ya
nyumba yako hakuna chakula, unafahamu mara ya mwisho ulipokutana na hali
kama hiyo ulifanya nini!
Katika maisha ya kindoa na uhusiano wa kimapenzi, siku hizi kumekuwa na
misemo mingi inayomaanisha kuwa fedha ni kitu cha msingi sana
unapozungumzia kuhusu msichana kuishi kinyumba na mvulana.
‘Hapendwi mtu hapa pochi tu’, Mapenzi Bongo?, Acha maneno hata kwenye kanga yapo na mengine kadha wa kadha. Ni misemo ya watoto wa mjini inayoonyesha jinsi gani watu wanatanguliza fedha kwanza katika suala la maisha ya uhusiano wa kimapenzi au ndoa.
‘Hapendwi mtu hapa pochi tu’, Mapenzi Bongo?, Acha maneno hata kwenye kanga yapo na mengine kadha wa kadha. Ni misemo ya watoto wa mjini inayoonyesha jinsi gani watu wanatanguliza fedha kwanza katika suala la maisha ya uhusiano wa kimapenzi au ndoa.
Hii siyo mara yangu ya kwanza kuzungumzia suala hili. Nimesema mara
nyingi kwamba ni kweli, katika maisha ya sasa, ni vigumu sana
kutoihusisha fedha katika mapenzi, kwamba uwepo wake, unasaidia kwa
kiwango kikubwa kuimarika kwa penzi lenyewe.
Ukitembea na kuzungumza na vijana wengi wa sasa wanakuambia ukiwa na
pesa ‘utang’oa’ demu wa aina yeyote, kwa sababu huwa hawana ujanja
panapo mapesa. Na hili linadhihirishwa na wengi wanapobadili wanawake
kwa sababu ya uwezo wao wa kifedha.
Na hata wanawake wenyewe nao wanaonekana kuhamasika sana kukutana na
mvulana mwenye fedha, kama ambavyo hata vijana wa kiume nao siku hizi
hupenda wadada wenye nazo.
Lakini ninataka kusema jambo moja ili kila mmoja limkae akilini mwake,
kwamba pamoja na ukweli huu wa fedha kuchagiza sana mapenzi, lakini
mapenzi ya kweli yapo na yana nguvu kubwa kuliko kawaida.Uthibitisho
wa hili, chunguza au jichunguze mwenyewe unapofuatilia penzi la pesa.
Kwa wavulana, wana pesa, wana mke nyumbani (wanayempenda) utawasikia
wanatamka maneno kama haya “leo nataka mlupo wa maana nikapumzike nao”
Na akina dada nao, wanaoishi na waume wawapendao unaweza kuwasikia
wakisema “Sijui nimpate wapi zoba ajiingize nipate hela ya saluni.”Maana
ya kauli ya wawili hawa ni kuwa wako tayari kutumia au kutumiwa na
fedha ili kukidhi matamanio yao ya kimwili na kimahitaji. Mvulana
atataka aifurahishe nafsi yake kwa kumpata msichana kwa fedha, wakati
mdada atahitaji fedha kwa kuutumia mwili wake ili mradi tu apate
kutimiza mahitaji yake.
Lakini jambo tunaloweza kujifunza ni kwamba wote wana wenza wao ambao
hawahitaji fedha ili kufurahi nao. Wanaume wenye wapenzi wao, huogopa
kuwapa fedha zenye mlengo wa kuhonga.
Pesa hutajwa kwenye maendeleo baina ya wawili na siyo mtaji wa
kumalizana kiu ya kimahaba. Unaweza kumkuta msichana mrembo anatoka na
mtu mwenye fedha, lakini ukimchunguza undani wake, unakuta kuwa huko
anakotoka, anaye mpenzi wake wa dhati kabisa, ambaye wakati mwingine
huwa anaelewa uhusiano wa mpenziwe huyo na kibopa.
Ninachotaka wote kuamini ni kuwa hakuna kiwango cha fedha kinachoweza
kununua mapenzi, isipokuwa mapenzi ya dhati yanaweza kukusanya kiasi
chote cha fedha kilichopo na kukileta ndani.
Pesa ni mbwembwe tu, lakini hazina ubavu wowote wa kudhibiti penzi.
Ndiyo maana unawaona wanawake walioolewa na matajiri wanatoka nje, tena
na magari yenye vioo vya giza, wanaenda kuupa moyo burudani huko kusiko
na fedha.
Msichana atakimbia ndoa ya kijana
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment