tiko
tiko
MSHEHERESHAJI wa
onyesho la Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ kumpongeza mwimbaji
kiongozi Luiza Mbutu kutimiza miaka 16 ya kuifanyia kazi mfululizo bila
kuhama, Sakina Lyoka, Jumamosi iliyopita alimkera mgeni rasmi, Waziri wa
Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Fenela Mkangara baada ya kukosea
kutamka vizuri cheo chake.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Fenela Mkangara (kushoto) akiwa na Luiza Mbutu.
Mtangazaji huyo wa televisheni, wakati akimkaribisha, alimtambulisha
kama Waziri wa Utamaduni, kitu ambacho kilimkera kiasi cha kumnyang’anya
kipaza sauti ili kumsahihisha.
“Jamani mimi naitwa Fenela Mkangara, ni Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo na siyo Waziri wa Utamaduni kama alivyonitambulisha
huyu Mc,” alisema Waziri huyo ambaye baadaye alimpongeza Luiza kwa
kudumu kwa muda wote bila kuhama na kuonyesha nidhamu kazini.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment