tiko
tiko
"....Kwenye hii dunia ukizaliwa mpaka unakufa lazima kuna mitihani
binaadam utaipitia ,toka nimezaliwa me Amanda mpaka leo hii nimepitia
mitihani migumu sana ...lakini katika mitihani yooote hakuna mtihani
unaokataa kuondoka ndani ya kichwa changu kama ule niliyowahi kufiwa na
mchumba angu tena ghafla nusu saa baada ya kuongea nae na kuniachia
mimba then mtoto akafia tumboni....
Kiukweli nilijifunza sana na ndio maana mpaka leo uwa naamini kila
mwanamke ameumbwa kutoka kwenye ubavu wa mwanaume hivyo ukiona uliyenae
anakuumiza na kukuliza tena akiwa ajali maumivu yako nakuapia huo siyo
ubavu wako,futa machozi kisha muombe mungu akuletee ubavu wako...
(John Abraham (pichani hapo juu) ni star wa movie za kihindi lkn
ni mwanaume aliyefanana kama mapacha na mwanaume aliyefariki akaniacha
na maumivu co yeye alikuwa amechanganya mgiriki na mbongo..
Haya niliyonayo mpaka muda huu kila nikimkumbuka n niliamua
kuchana pics zake zote na kubaki moja iliyofichwa na ndugu zng mpk leo
kwa kujaribu kunipunguzia majonzi lkn naamini hayatokuja kufutika kamwe)
Hakuwa ubavu wangu ndio maana naamini mungu alimchukua mapema
sana...ninachomkumbuka zaidi mwenzenu sikuwahi julia coz alikuwa hapendi
aone machozi yng,nilikuwa nacheka muda wote n nakumbuka niliwahi kulia
mara moja tu tena baada ya kuona tumbo lng linazidi lkn alinielewesha
nikijifungua basi nitarudi kama nilivyokuwa lkn aliondoka na mtoto
wake....nimemkumbuka...siku yng imekua mbaya sana kwangu leo wallah
..."- Mwigizaji Amanda Poshi alimaliza kusimulia.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment