tiko
tiko
Na Makongoro Oging’, Issa Mnally/Uwazi
MTU mmoja anayeaminika kuwa ni Mtanzania, Robert John Mpwata (34)
anadaiwa kuuawa kwa kuwekewa sumu na mwili wake kukutwa chumbani kwake
katika Mji wa Shorten nchini Ujerumani siku chache zilizopita.
Habari kutoka kwa baadhi ya marafiki zake waliopo huko, zinasema Robert
aliyekuwa mwanamichezo aliyecheza sarakasi, karate na judo, aliwasiliana
nao kwa njia ya simu mara kwa mara na walipata taarifa za kifo chake
siku saba ya kufariki dunia.
Inadaiwa kabla ya kifo cha mwanamichezo huyo, alikuwa akiwasiliana
vizuri na wenzake, lakini umauti wa ghafla uliomkuta na mazingira yake,
unawapa hofu kuwa huenda alifariki baada ya kuwekewa sumu.
Inadaiwa kuwa Februari 8, mwaka huu ilikuwa ni siku waliyotakiwa kufanya onyesho, kitu ambacho kiiwafanya wawe na mawasiliano ya mara kwa mara.
Inadaiwa kuwa Februari 8, mwaka huu ilikuwa ni siku waliyotakiwa kufanya onyesho, kitu ambacho kiiwafanya wawe na mawasiliano ya mara kwa mara.
Mwandishi wa habari hii aliwasiliana na ubalozi wa Tanzania nchini
Ujerumani, ambako mfanyakazi mmoja aliyekataa kutajwa jina lake kwa vile
siyo msemaji, alikiri kusikia taarifa hizo, lakini akasema inakuwa
vigumu kwao kutoa msaada kwa vile taarifa isiyo rasmi inasema marehemu
alikutwa na vielelezo vinavyomtambulisha kuwa ni mtu wa Somalia.
Robert John Mpwata akiwa na mke wake.
Naye Mwenyekiti wa umoja wa Watanzania nchini humo, Mfundo Peter Mfundo
alikiri kutokea kwa kifo hicho, kwani awali marehemu aliwaaga Watanzania
wenzake kuwa ataondoka kwenda nyumbani kwa mke wake.
“Mimi nilipata taarifa kutoka kwa rafiki yake wa karibu baada ya wiki
mbili tangu akutwe amefariki, hakuna anayejua kilichomuua maana serikali
bado haijatoa majibu. “Mpaka sasa bado tunasubiri kutatokea nini na
hata kama ikitokea tupewe maiti kuisafirisha ni kazi kwani ni zaidi ya
shilingi milioni 12, nimewasiliana na baba yake anasema hana nauli ya
kumleta huko.
“Robert alikuja hapa katika shughuli za sanaa na alimuoa Mjerumani
aliyezaa naye mtoto Daniel ambaye ana umri wa miezi minne,” alisema
kiongozi huyo.Kwa mujibu wa Peter, mke wa marehemu aliwaambia kwamba
angependa amzike mumewe nchini humo ili iwe rahisi kwa mtoto wake kuhani
kaburi lake.
John Mpwata (65), baba mzazi wa marehemu akiwa nyumbani kwake Manzese
Kilimahewa jijini Dar, alisema taarifa za kifo hicho
zimemuumiza.“Mwanangu aliondoka mwaka 2007 kutafuta maisha huko
Ujerumani na kwa mara ya mwisho niliongea naye Desemba 22, mwaka jana,
aliniambia atakuja nyumbani na mkewe Mzungu hivi karibuni baada ya
mwanaye Daniel kuanza kutembea.
“Lakini cha kushangaza hivi karibuni nimepata taarifa ya kifo chake,
sina jinsi maana nimeambiwa uwezekano wa mwili kuletwa ni mdogo na
ningependa kwenda kumzika lakini sina milioni 2.5 za nauli, ninawaomba
Watanzania wanisaidie nikamzike mwanangu,” alisema na kutaja namba zake
za simu kuwa ni 0689 476408 au 0713 432088.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment