tiko
tiko
KATIKA Live Chumba cha Habari cha Global Publishers, leo hii tunaye Miss Universe 2014, Nale Boniface ambaye ameweka wazi siri ya urembo na kusema kuwa kujiamini ni sifa mojawapo ya kumfanya mtu aitangaze vizuri nchi yake.
Presenta wa Global TV Online, Pamela Daffa akiongea na mwakilishi wa Miss Universe Tanzania 2014, Nale Boniface.
Katika mahojiano na safu hii huku akirekodiwa na timu nzima ya Global TV
Online ambapo tayari yamerushwa jana kupitia tovuti ya www.globaltvtz.com kwenye Kipindi cha Mtu Kati, Nale alifunguka;
Mwandishi: Ulianzia wapi mpaka ukafikia kushiriki Miss Universe?

Nale: Sijaanza jana, Mwaka 2013 nilianzia Miss Tanzania ambapo nilikuwa
Miss Chang’ombe, 2013 nikawa Miss Temeke na kufanikiwa kuingia Miss
Tanzania, nikafika mpaka 15 bora na kuwa Top Model, nikawa Balozi wa
Marie Stopes Tanzania sikukata tamaa nikaingia Miss Universe na
kuiwakilisha nchi katika Miss Earth na pia nikapata nafasi ya kushiriki
Miss Universe pale Florida Miami.
Mwandishi: Miss Earth ni nini?
Nale: Ni shindano zima la urembo ambapo timu nzima ya Miss Earth inatusaidia sisi warembo kufanya kazi za jamii na ndiyo maana timu yake nzima ina shughulika na masuala ya mazingira na namna ya kuziwakilisha nchi zetu katika masuala ya utalii.

Mwandishi: Ni vigezo gani huwa wanaangalia pindi mtu anapotaka kushiriki Miss Universe?
Nale: Sanasana wanachokiangalia ni kujiamini na uzuri, yaani lazima uwe unajiamini ndiyo kigezo cha kwanza uzuri baadaye watu wanaangalia moyo wako na namna ambavyo utaiwakilisha nchi yako.

Mwandishi: Inaonekana Miss Universe haina nguvu kama Miss Tanzania, unahisi tatizo ni nini?
Nale: Hamna tatizo lakini Miss Tanzania ilikuwa kabla ya Miss Universe na kitu chochote kikubwa lazima kianzie chini.

Mwandishi: Tukimzungumzia yule Mnigeria na nafasi aliyoshika. Je, walikuwa wanaangalia vigezo gani?
Nale: Hiyo nafasi ilikuwa ni sisi warembo wenyewe tulikuwa tunataja watu, ikatokea amepata kura nyingi lakini inategemea aliishi vipi na watu.

Mwandishi: Tumezoea kuona warembo wanadanganya umri wao, tatizo ni nini?
Nale: Mimi nina miaka 23. Hapo kwenye kudanganya siwezi kuliongelea sana lakini naweza nikasema ni fasheni, unajua mtu anatamani ushiriki lakini anashindwa kupata nafasi ndiyo maana baadhi hudanganya umri.

Mwandishi: Unazungumziaje suala la Miss Tanzania kufungiwa?
Nale: Kwakweli limenigusa, ndiyo makosa yametokea lakini wasingeifungia kwa sababu kuna warembo wengi wana ndoto za kutimiza malengo yao .

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment