tiko
tiko
Mwigizaji
wa toka kitambo, Davina Yahaya ‘Davina’, amesema kamwe hatokuja kusahau
mateso aliyowahi kuyapata akiwa Gereza la Segerea ambapo alikaa kwa
siku tatu.
Akipiga stori na GPL, Davina alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa
mwaka 2012 ambapo ilikuwa ni tatizo la kifamilia lililosababisha
kutupiwa huko japokuwa hakuweza kuliweka hadharani kwakuwa bado lipo
mikononi mwa sheria.
“Huwa natokwa machozi na kamwe sitokuja kusahau mateso niliyoyapata
Segerea. Nilikuwa kwa siku tatu lakini niliona kama mwezi, hali ya hewa,
sehemu ya kulala zilikuwa mbaya sana, wingi wa watu na sikupata hata
nafasi ya kulala zaidi ya kukesha nikilia,” alisema Davina.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment