tiko
tiko

Kiungo wa timu ya taifa ya Ivory Coast ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo Yaya Toure hapo jana alizua hofu kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kulazimika kukosa mazoezi ya timu hiyo baada ya kupata jeraha .
Toure alilazimika kukatisha mazoezi yake na kukaa nje akiugulia kwa maumivu huku madaktari wa timu hiyo wakimtibia taswira ambayo ilizua hofu kubwa ya kiungo huyo kushindwa kuichezea timu yake kwenye mchezo wa kwanza wa michuano hiyo kwa timu hii .

Yaya
 Toure akitazamwa na daktari wa timu na kocha wake Herve Renard baada ya
 kuumia kwenye mazoezi ya kwanza nchini Equatorial Guinea.
Bado haijafahamika kama Toure ataweza kufanya mazoezi kwa siku zilizosalia kabla ya mchezo na haijaweza kufahamika kama atakuwepo wakati Ivory Coast ikicheza na Guinea .
tiko
tiko


Post a Comment