tiko
tiko
Kocha wa zamani wa Fc Barcelona Pep Guardiola ameingilia kati sakata la mchezaji nyota wa timu hiyo Lionel Messi kutaka kuhama baada ya kufanya mazungumzo maalum na mchezaji huyo na kumpa ushauri .
Guardiola alifanya mazungumzo hayo kupitia njia ya simu ambapo alimshauri Messi kuwa hakuna ti mu nzuri ya kuchezea zaidi ya Barcelona katika hatua aliyoko sasa hivi katika maisha yake kama mchezaji .
Guardiola pia amemshauri Messi kwamba anapaswa kuwa na Imani na kocha wa sasa wa Barcelona Luis Enrique na kazi anayoifanya kwani hakuakuwa na maendeleo katika klabu hiyo endapo kocha huyo atafukuzwa .
Messi kwa muda mrefu sasa amevumishwa kuwa na mpango wa kuihama Barcelona tetesi ambazo zilizidi mwanzoni mwa wiki iliyopita kwenye hafla ya utoaji tuzo za wachezaji bora wa dunia Ballon D’or ambapo mchezaji huyu alisema kuwa hafahamu atakuwa wapi hapo baadae kwani kwenye soka lolote laweza kutokea .
Guardiola amemuasa Messi kuwa anapswa kukumbuka kile anachomaanisha kwa Barcelona na mahali ambako klabu hiyo imemfikisha kama mchezaji na kama mtu binafsi huku pia akimkumbusha jinsi ambavyo kila mtu ndani ya Barcelona anavyomuunga mkono ambapo alimsihi kuwa hakuna mahali kokote atakakopata alichokipata zaidi ya Barcelona .
Messi siku zote amekuwa msikivu kwa watu anaowaheshimu na mmoja wao ni kocha Pep Guardiola ambaye chini yake Muargentina huyo alipata mafanikio makubwa katika ngazi ya klabu .
tiko
tiko
Post a Comment