tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Pichani ni Daktari
wa Zahanati ya Nyankumbu iliyopo mkoani Geita Josephat Msafiri akipata
kichapo baada ya kukutwa akilewa muda wa kazi-picha kutoka maktaba ya
malunde1 blog |
Mwandishi
wa Gazeti la Mwananchi Mkoa wa Geita Jackline Masinde,ametishiwa kuuawa
na Daktari wa Zahanati ya Nyankumbu iliyopo mkoani Geita Josephat
Msafiri.
Inaelezwa kuwa tarehe 23 Desemba mwaka
jana Mwandishi huyo aliripoti taarifa za Daktari huyo kuwafungia nje
wagonjwa kisha kwenda kulewa pombe na kuacha wagonjwa wakiwa wamezidiwa katika kituo alichokuwa akifanyia kazi cha Nyakabale hapo awali .
Hali hiyo ilisababisha wagonjwa kumfuata baa alikokuwa akilewa pombe kisha kumwadhibu kwa viboko ,ambapo taarifa hiyo ilisababisha daktari kuvuliwa
madaraka yake kisha kuhamishwa kituo chake cha kazi na kupelekwa kituo
cha Nyankumbu na mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi wa Halmashauri ya mji
wa Geita Magreth Nakainga.
Mwandishi
huyo alisema juzi majira ya saa 5:23 asubuhi alimpigia Daktari huyo
ikiwa nimoja wa wajibu wake wa kazi akihitaji taarifa za kitaalam kuhusu
madhara ya sumu ya Zebaki ofisini kwake .
“Nilimpigia simu daktari nikihitaji taarifa za madhara ya sumu ya Zebaki ,alipokea simu na kuanza kunitolea lugha za matusi (tunazihifadhi kwa sababu ya maadili) huku akinitishia kuniua kwa kusema "nikionana nawewe sehemu yoyote haki ya mungu nakuua”,alimnukuu Daktari huyo.
Alisema
alipomuhoji kwanini anamtishia kumuua,daktari huyo alisema ana uchungu
na taarifa alizozitangaza nchi nzima kuhusu yeye kupigwa na wagonjwa
,kuwa imemuathiri katika maisha yake.
Mwandishi
huyo alisema kuwa kauli hiyo ya Daktari ilimpa mashaka kisha kutoa
taarifa kituo cha Polisi cha Wilaya ya Geita mkoani humo na kufungua
kesi namba GE/RB/366/2015 ya kutishiwa kuuawa kwa njia ya mtandao.
"Niliamua
kutoa taarifa polisi na mtuhumiwa mpaka sasa amekamatwa ,alipohojiwa
alikiri kufanya kosa na kuomba msamaha mbele ya polisi"alisema Masinde.
Mwandishi
huyo wa habari sasa yuko katika wakati mgumu kutokana na kufichua maovu
mengi katika jamii na amekuwa akipata vitisho mbalimbali kutoka kwa
baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakimtishia kumpeleka mahakamani kwa
kile kinachoelezwa kuwa anawaandika vibaya,huku pia akinusurika kupigwa
na kuharibiwa vifaa vyake vya kazi.
Na Valence Robert-Dunia Kiganjani blog Geita
Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu
tiko
tiko
Post a Comment