tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
WAKAZI
wa kijiji cha Burunde kata ya Karitu wilayani Nzega mkoani Tabora,
wamewapiga, kuwaua na kuwachoma moto watu watatu kwa tuhuma za kushiriki
kumuua Helena Abel na kumjeruhi mume wake, Said Msoma.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Juma
Bwile alisema tukio hilo limetokea Januari 15 mwaka huu.
Alisema
kuwa Januari 12 mwaka huu Helena Abel na mume wake Said Msoma
walivamiwa katika tukio hilo .Helena aliuawa na Said Msoma alifanikiwa
kumjeruhi mmoja wa wahalifu hao ambaye alikimbia.
Kamanda
Juma alisema kuwa wananchi hao walifanya doria na kumkamata mhalifu
huyo aliyejeruhiwa ambaye anaitwa Mainda Mahila na kuanza kumhoji
kuhusika na mauaji hayo na kukiri kufanya hivyo.
Bwile
alisema kuwa mtuhumiwa huyo aliwaeleza wananchi hao kuwa mauaji hayo
alifanya kwa kuagizwa na Mama Zainabu Hamis pamoja na mtoto wake
aliyefahamika kwa jina la Zena Yasoda.
Wananchi hao waliwapata watuhumiwa hao wawili kisha kuanza kuwapiga hadi kufa na baadaye kuwachoma moto.
Wakati
huo huo mkazi mmoja wa kijiji cha Muhugi kata ya Muhugi wilayani Nzega
Chenge Kasinki (75) aliuawa na watu wasiofahamika baada ya kuvamiwa
nyumbani kwake.
tiko
tiko
Post a Comment