tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
JESHI
la Polisi mkoani Kagera linawashikilia watu tisa kwa tuhuma za mauaji
katika matukio mawili tofauti wakiwemo mume na mke waliomuua mganga wa
jadi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Henry
Mwaibambe, alisema tukio la kwanza lilitokea saa 3:00 usiku wa Januari
14 mwaka huu katika kata ya Bugarama wilayani Ngara ambapo mganga wa
jadi, Alfaxad John ( 36 ) akiwa anaendesha pikipiki yake yenye namba za
usajili T.237 CDK alikufa baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali.
Alisema
inaaminika mganga huyo alipigwa na shoka kichwani na kusababisha kichwa
kugawanyika sehemu mbili na shingo kutenganishwa.
Alisema
siku mbili kabla ya tukio hilo la mauaji John aliibiwa mbuzi watano
nyumbani kwake, aliwaona wezi lakini hakutoka nje ili kulinda usalama
wake.
Baada
ya muda alipata ujumbe wa simu ya mkononi kutoka kwa mpenzi wake
ukisema “pole mpenzi nipo pamoja na wewe ungetoka nje ili kukabiliana na
wezi hao ungeuawa”.
Aliwataja
watuhumiwa wanaoshikiliwa kuwa ni Burhani Tutuleka (40 ) mwalimu wa
shule ya msingi Rwinyana iliyoko kata ya Bugarama na mkewe Madina
Khamisi (35).
Ingawa
chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana lakini mke wa mtuhumiwa
alikuwa anatibiwa na John na mumewe alikuwa akimtuhumu mganga huyo kuwa
ana uhusiano wa kimapenzi na mke wake.
Kamanda
Mwaibambe alisema tukio la pili lilitokea saa 8:30 usiku wa Januari 15
mwaka huu ambapo kundi la wahalifu wasiopungua 10 walimvamia na kumuua
Onesmo Mutta ( 24 ) mkazi wa Mtaa wa Katotorwansi kata ya Kashai
Manispaa ya Bukoba.
Alisema
katika tukio hilo wahalifu hao walivamia nyumba aliyokuwa akiishi Mutta
ambayo ilikuwa na wapangaji wengine na kuanza kuwapiga na kudai
kupatiwa fedha huku wakiwa wamebeba mapanga na marungu.
Alisema
Mutta alichomwa na kitu chenye ncha kali kifuani upande wa kushoto na
kufa papo hapo. Alisema wapangaji wengine watatu na mke wa Mutta
walijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao.
Wahalifu
hao walifanikiwa kuiba vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh 400,000.
Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Philipina Onesmo mke wa Mutta ,Edwin
Haipolite (23 ) mjasiriamali, Adelene Simon (27 )n a Denice Gervas.
Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu
tiko
tiko
Post a Comment