tiko
tiko

Wakati mshambuliaji wa Olympique Marseile Mario Lemina alipoitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Gabon alikataa katakata na sababu yake ilikuwa moja , hajihesabu kama raia wa Gabon baada ya kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa kwenye vijana wenye umri chini ya miaka 20 .
Pamoja na kuwa na asili ya Gabon , Lemina aligoma kuichezea Gbaon kwani anataka kuiwakilisha timu ya taifa ya Ufaransa na katika hilo anaungana na wachezaji wengine wanaounda orodha ndefu ya wachezaji ambao wakati huu wa michuano ya Afcon labda tungeweza kuwaona wakichezea mataifa ya Afrika badala ya ulaya .

Mario Lemina ambaye ana asili ya Gabon alikataa kuihcezea timu hiyo kwa kuwa anataka kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa .
Michuano ya AFCON ilianza rasmi mwaka 1957 lakini Msumbiji haikuwa na ligi kipindi hicho na hawakuwa na timu ya taifa ambayo ingeweza kucheza mechi za kimataifa hali iliyosababisha Coluna na Eusebio kuchukuliwa kwenda kuichezea Ureno .
Mchezaji wa zamani wa Barcelona na Glasgow Celtics na Manchester United Henrik Larson angeweza kuitumikia timu ya taifa ya Cape Verde lakini nafasi hiyo haikuwahi kutokea . Larson ana asili ya visiwani humo kupitia kwa baba yake mzazi na mwenyewe anakiri kuwa angeweza kuichezea Cape Verde lakini hakuna aliyewahi kuleta wazo hilo na pia alizaliwa na kukulia Sweden hivyo siku zote amejiona kuwa na asili ya taifa hilo la ulaya .

Luis Nani ni mchezaji mwingine ambaye amezaliwa nchini Cape Verde lakini leo hii ana uraia wa Ureno.
Mfano wa ugumu wa maamuzi kama haya umeonekana kwenye familia ya kina Boateng ambako Kevin Prince na Mdogo wake Jerome wamejikuta wakiwakilisha mataifa tofauti . Wote wawili wakiwa wameichezea Ujerumani kwenye vikosi vya timu za vijana Kevin Prince aliamua kuihcezea Ghana huku Jerome akibaki na Ujerumani ambayo mwaka jana alikuwa moja kati ya wachezaji waliotwaa kombe la dunia wakiwa na timu hiyo .

Ndugu wawili Jerome pamoja na Kevin-Prince Boateng wana uraia wa Ujerumani na Ghana pamoja na kuwa na baba mmoja .
tiko
tiko








Post a Comment