tiko
tiko
Wanafunzi 48 wasichana wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari ya vipaji maalum ya Muungano wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamenusurika kifo baada ya bweni lao kuteketea kwa moto na vifaa vyao vyote.
Mwenyekiti
wa bodi ya shule hiyo ya wananchi Mh Zawadiel Maruchu amesema, moto huo
ulianza kwenye bweni hilo kuanzia saa moja usiku wakati wanafunzi
wakijiandaa kupata chakula lakini hamna aliyejeruhiwa.
Mh
Maruchu amevipongeza vyombo vya ulinzi, zima moto na wananchi kwa
ushirikiano wao mkubwa uliofanikisha kuzimwa kwa moto huo ambao
umetekeza vifaa vyote ingawa kuna mabaki kidogo ya nguo.
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Moshi Bw Flugence Mponji amesema,
wanafunzi wa kidato hicho wamerudishwa nyumbani kwao kwa wiki moja
wakati serikali inafanya juhudi za haraka kuwatafutia malazi.
Wanafunzi
wa shule hiyo wameiomba serikali iimarishe ulinzi na kuweka uzio wa
shule na kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo ambalo limeacha
maswali mengi miongoni mwa wananchi wa kata ya kilema kusini.
Wazazi
wa wanafunzi hao wameiomba serikali iweke miundo mbinu yenye hadhi ya
shule hiyo kuwa ya bweni ya wasichana wa vipaji maalum kuliko hali
ilivyo sasa ambayo mazingira yake ni hatarishi.
tiko
tiko
Post a Comment