Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Arsenal yaifanyia Man City kitu mbaya.

tiko tiko
IHN SPT 180115-05

Katika matokeo yua kushangaza yaliyotokea mwishoni mwa wiki hii klabu ya Arsenal imewafunga mabingwa watetezi wa ligi ya England Manchester City kwenye uwanja wao wa nyumbani kwa matokeo ya 2-0.
Huku wengi wakitegemea kuishuhudia Arsenal ikifungwa , matokeo yalikwenda kinyume baada ya Santi Cazorla kuifungia timu yake bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati baada ya nahodha wa City Vincent Kompany kumuangusha Nacho Monreal kwenye eneo la hatari .
Wakati wengi wakisubiri kuiona City ikirudi mchezoni na kufunga bao la kusawazisha hali ilizidi kuwa mbaya baada ya mshambuliaji Olivier Giroud kufunga bao la pili na kuua kabisa matumaini ya City .
Santi Cazorla akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la kwanza.
Santi Cazorla akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la kwanza.
Matokeo haya yamemfaidisha zaidi Chelsea ambao wameendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi tano wakiwa wamekusannya pointi 52 huku Man City wakiwa na pointi 47 .
Arsenal kwa upande wao wamechupa hadi nafasi ya tano nyuma ya Manchester United wakiwa na pointi 39 , tofauti ya pointi moja pekee dhidi ya mashetani wekundu .
Katika mchezo mwingine uliopigwa hii leo West Ham United waliwafunga Hull City kwa matokeo ya 3-0 wafungaji wakiwa Andy Caroll , Morgan Amalfitano na Stewart Downing.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top