Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Eto’o Kurudi Italia.

tiko tiko
etoo

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto’o Fils anakaribia kuihama klabu ya Everton ambapo inaarifiwa kuwa atajiunga na Sampdoria ya nchini Italia ndani ya saa chache zijazo .
Eto’o alisaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Everton lakini amekuwa akisugua benchi baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza hali ambayo imeshawishi kuhama na kwenda mahali ambako atakuwa akipata nafasi ya kucheza .
Msimu uliopita Eto'o aliichezea Chelsea na sasa anakaribia kujiunga na Sampdoria ya Italia .
Msimu uliopita Eto’o aliichezea Chelsea na sasa anakaribia kujiunga na Sampdoria ya Italia .
Eto’o ameshindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Everton baada ya kocha Roberto Martinez kupendelea kuwatumia Romelu Lukaku na James Naismith ambao wamekuwa wakiongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo .
Eto’o alijiunga na Everton baada ya kuichezea klabu ya Chelsea kwa msimu mmoja akiwa anatokea nchini Urusi ambako alicheza Anzhi Makhachkala ya nchini humo .
Mshambuliaji huyu alitangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Cameroon mara baada ya michuano ya kombe la dunia iliyopigw amwaka jana nchini Brazil.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top