tiko
tiko
Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limefanikiwa kudhibiti wananchi waliobeba madumu wakitaka kuiba mafuta baada ya lori la mafuta kuanguna katika eneo la Mikese mkoani Morogoro.
Dereva
wa lori Deogras John hilo akizungumzia tuki hilo la ajali amesema
chanzo cha ajali alikua akijaribu kukwepa mtoto aliekua akivuka barabara
ndipo gari ikapoteza mweleko na kupinduka mara kadhaa ambapo wananchi
walijitokeza na madumu na kuanza kuiba mafuta.
Nao
wananchi wa eneo la Mikese katika hali iso ya kawaida wamelalamikia
jeshi la polisi kuwazuia kuiba mafuta na kueleza kuwa wamefanya kazi ya
kumuokoa dereva kwa kumtoa kwenye gari na hivyo walipaswa kuchukua
mafuta kama ujira wao.
tiko
tiko
Post a Comment