tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
HALI ni
mbaya! Wakati suala la ajira likiwa bado ni kitendawili kikubwa kwa
serikali, Jiji la Dar hivi sasa linatisha, baada ya watu kubuni mtindo
mpya wa kujipatia fedha kwa kujihusisha na biashara haramu ya ngono
katika maeneo yanayotambulika kufanya shughuli nyingine halali, Risasi
Jumamosi lina mkanda mzima.
Mhudumu wa saluni ya kuchua akitweta mara baada ya kunaswa na OFM akijihusisha na biashara haramu ya ngono.
Makachero wa kitengo
maalum cha Global Publishers cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) walifanya
uchunguzi na kugundua kuwa zipo saluni nyingi jijini Dar
zinazojishughulisha na biashara ya massage (kuchua) lakini ndani yake
wahudumu wanajiuza hadi miili ambapo wateja wakubwa ni waume za watu na
vigogo serikalini.
Kikosi kazi cha OFM kikimtaiti mhudumu huyo.
TUKIO BICHI
Hivi karibuni OFM
walipokea simu kutoka kwa mmoja wa wanawake aliyedai kuchoshwa na
shughuli zinazofanyika katika saluni moja ya kuchua (massage, jina
linahifadhiwa kwa sasa) iliyopo katika eneo la Kinondoni-Morocco, Dar.
Mhudumu huyo mwenye asili ya kisomali akitinga viwalo mara baada ya kunaswa katika mtego wa OFM.
“Jamani nipo hapa nje,
nimemfuatilia mume wangu, maana kila siku nasikia huwa anaonekana hapa,
hii ni saluni ya kuchua, lakini humo ndani wale wahudumu ni makahaba,
wanajiuza tena wanafanyia humohumo ndani, naombeni mje, nataka
kufumania,” chanzo chetu kiliongea kwa hasira na uchungu.
...Huyu hapa ndio mhudumu mwenyewe.
OFM MZIGONI
Kama ilivyo kawaida ya
OFM kutodharau wito wowote unaohusiana na uvunjaji wa maadili, uonevu na
uhalifu, kikosi kilipangwa harakaharaka na kwa kutumia pikipiki
ziendazo kasi, zikafika eneo la tukio katika muda muafaka, kwani difenda
la polisi, nayo ilionekana ikiingia eneo hilo kuitikia wito wa raia
wema.
Baadhi ya vifaa vya kufanyia masaji vikiwa mezani.
KABAAAH!
Ndani ya saluni hiyo, OFM
ilishuhudia mhudumu wa mapokezi ambaye baada ya kuonyeshwa vitambulisho
vya askari wa Jeshi la Polisi, alinywea na kuwaruhusu kupekua chumba
kimoja baada ya kingine, ili kujionea kama kweli nyumba hiyo ilikuwa
ikijihusisha na masuala ya saluni ya uchuaji pekee na siyo vinginevyo.
Moja ya vitanda vinavyotumiwa kwa ajili ya biashara ya ngono kwa wateja wanaofika katika saluni hiyo.
Katika chumba cha kwanza,
askari hao walimkuta mwanaume mmoja akiwa uchi wa nyama, lakini
mwanamke aliyekuwa naye akiwa amevaa nguo zake, kitu kilichoashiria kuwa
tayari ‘mchezo ulishafanyika’.
Katika hali
isiyotarajiwa, baada ya kupitia vyumba vingine vinne na kuvikuta tupu,
kilichofuata, OFM walishuhudia mwanamke mwenye asili ya Kisomali akiwa
uchi na mwanaume wake, dalili zote zikionyesha kuwa walikuwa wakijiandaa
kufanya uzinzi.
WAZINZI WAJITETEA
Baada ya kuwakuta katika
hali hiyo, kiongozi wa askari hao, (jina kapuni) aliwauliza kama hiyo
ndiyo biashara ya masaji waliyopata kibali cha kuifanya, lakini
wakabakia kujiumauma pasipo kutoa jibu la kueleweka.
Binti huyo wa Kisomali,
ghafla aliibuka na kuanza kuomba msamaha kwa kitendo hicho, akidai
maisha magumu wanayoishi, ndiyo yanayosababisha waifanye biashara hiyo.
KUMBE ANA MTOTO
Lakini la kushangaza
zaidi, ni pale mwanamke huyo alipodai kuwa nyumbani alikotoka, ambako
ameolewa, pia alimuacha mwanaye mwenye umri wa miezi minne.
“Nisameheni jamani, mimi
ni mke wa mtu na isitoshe nimeacha kichanga nyumbani, ni shida tu ndiyo
imenileta hapa,” alisikika akiomba mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa
jina moja la Salma.
Mwanaume aliyekutwa naye,
alipoulizwa biashara hiyo inafanyika kwa bei gani, alisema makubaliano
yake na mwanamke huyo, ni kutoa kiasi cha shilingi elfu sitini kwa tendo
moja!
OFM iliondoka eneo hilo
baada ya askari hao kuwapakiza katika karandinga wanawake wanne na
wanaume wawili tayari kwa safari ya kituoni kwa ajili ya hatua zaidi za
kisheria.
Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu
tiko
tiko
Post a Comment