tiko
tiko
Dk. Shukuru
Kibwana ambaye ni daktari katika wodi ya watoto ya hospitali ya rufaa
Bugando, amesema timu ya madaktari wa upasuaji na wataalamu wengine
wamefanya kila lililowezekana kuokoa maisha ya pacha hao walioungana
lakini haikuwezekana na kuongeza kuwa kabla ya upasuaji, mapacha hao
walitakiwa kupitia tomografia ( CT ) na kufanya kipimo cha ultra sound
ili kujua kama watoto hao wameungana baadhi ya maeneo na viungo muhimu.
Dk. Kibwana
amesema watoto hao licha ya kuungana, madaktari bingwa wa hospitali hiyo
wamegundua kuwa viungo vyao vingi vya mwili vilikuwa vikijitegemea,
kila mmoja alikuwa na figo yake, ini na moyo wake huku muuguzi wa zamu
katika wodi ya watoto Sembosah Hiza akieleza kuwa hali ya pacha hao
ilianza kubadilika jana mchana jambo lililokwamisha rufaa yao ya kwenda
hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi na uchunguzi.
Agosti 6 mwaka
jana mkazi wa katoro wilayani Geita Neema Luswetura alijifungua watoto
wakiwa wameungana sehemu ya kifua na tumbo wakiwa na uzito wa kilo 5.1
hata hivyo walifariki muda mfupi baadaye na mwishoni mwa mwaka jana
hospitali ya Apollo nchini India ilitangaza kufanikiwa kutenganisha
mapacha waliokuwa wameungana kutoka Tanzania katika upasuaji uliochukua
saa 11 na wataalamu 50.
tiko
tiko
Post a Comment