tiko
tiko
Jeshi
la Polisi la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA)linamshikilia raia wa Kuwait kwa tuhuma za kukutwa na viumbe hai
aina ya Kenge 149 wenye thamani ya Sh 6.3 milioni.
Kamanda
wa Polisi wa JNIA, Khamis Suleiman alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni
Hussain Ahmed Ally Mansour(34), raia wa Kuwait ambaye alikamatwa
uwanjani hapo jana majira ya saa 5 usiku wakati akijiandaa na safari
ya kuelekea nchini Kuwait kupitia Dubai na Shirika la Ndege la
Emirates .
Kamanda
Selemani alisema Mansour alikamatwa na wanyama hao ambao aliwahifadhi
kwenye mifuko midogo midogo ilivyowekwa katika begi kubwa lenye rangi
nyeusi.
“Kenge
waliwekwa kwenye mifuko midogo midogo 15 na kila mmoja kuna kenge 15 na
mifuko mingine walikaa wawili,”alisema kamanda Selemani.
Alisema kati ya Kenge hao, 15 walikufa na walio hai walikuwa 134 ambao walikuwa wamefichwa kwenye mifuko hiyo.
Seleman
alisema wakati wanafanyiwa upekuzi ndipo walipogundua kuna vitu
ambavyo vinafanana na nyoka na kuamua kuwashirikisha wataalamu wa
maliasili ambao walibaini kuwa begi hilo lilikuwa na Kenge.
“Huyu
mtuhumiwa alikuja nchini Januari 6,alitiliwa mashaka na polisi wa JNIA
na tulimuamuru akae pembeni kwa upekuzi zaidi na kugundua anasafirisha
kenge bila Kibali,”alisema Selemani.
Selemani
alisema walipoendelea kumuhoji mtuhumiwa huyo alidai kuwa alikuja
nchini kwa ajili ya kuchukua viumbe aina ya ndege lakini baada ya
kuwakosa aliamua kubeba Kenge hao.
Kamanda
Selemani aliwaomba wananchi kuwa na uzalendo wa nchi yao wanapoona mtu
anasafirisha rasilimali za nchi watoe taarifa katika jeshi la polisi.
Alisema
polisi wataendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo ya mipakani na
viwanja vya ndege ili kudhibiti aina hiyo ya utoroshaji wa nyara.
Julai
31, mwaka jana raia wa Vietnam, Dong Van (47) naye alikamatwa
uwanjani hapo akiwa na meno 65 na kucha 447 za simba zenye thamani ya
Sh189.4 milioni.
tiko
tiko
Post a Comment