tiko
tiko
MKAZI wa Dodoma, Ramadhan Zuber ambaye alikuwa abiria kwenye basi la Champion amefariki dunia akiwa safarini.
Akizungumza
na paparazi mjini Kibaha, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei
alisema kuwa Zuber (29) alikuwa akisafiri toka Dar es Salaam kwenda
Dodoma.
Kamanda
Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 16, saa 3:30 asubuhi
katika kijiji cha chamakweza wilaya ya Bagamoyo ambapo alibainika kuwa
ameshafariki dunia.
Alisema kuwa Zuber alikuwa amekaa kiti namba 3 kwenye basi hilo lenye namba za usajili T 909 BRA.
Chanzo
cha kifo hicho bado hakijafahamika. Alisema kuwa mwili wa marehemu
umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Tumbi kwa ajili ya uchunguzi.
tiko
tiko
Post a Comment