tiko
tiko
Mbunge wa Zitto Kabwe
leo amewahutubia Wananchi wa Mtwara kupitia mkutano ulioitishwa na
chama cha Wananchi CUF na kutoa ufafanuzi juu ya sakata la account ya
Tegeta Escrow.
Akizungumzia sakata hilo Zitto Kabwe
amesema kuwa baadhi ya viongozi waliohusika na sakata hilo ambao mpaka
hivi sasa hawajachukuliwa hatua yoyote lazima wachukuliwe kwa kuwa
serikali haiwezi kupingana na maazimio ya bunge.
“ Utekelezaji
wa maamuzi ya Bunge hauna mjadala… sisi kama Wabunge wa Kambi ya
Upinzani mwezi January kazi ya kwanza ni kupokea taarifa ya utekelezaji
wa maamuzi ya Bunge… Tunachokitaka kila mtu aliyehusika kwenye Escrow ni
lazima awajibike…“– Zitto Kabwe.
Sisi
lazima tuutumie mwaka 2015 kama mwaka wa uwajibishaji, mwaka wa
kuwajibishana… safari hii mmewawajibisha kwenye Seikali za Mitaa,
hongereni sana, tunaenda kuwawajibisha kwenye Serikali kuu sasa…”– Zitto Kabwe.
Unaweza kumsikiliza Mbunge huyo kwenye sauti hii hapa.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu,
niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na
facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment