tiko
tiko
Picha ya Maktaba ikumuonesha Frank Nyalusi (mwenye suti nyeupe) ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Iringa Mjini akiwa chini ya ulinzi wa Polisi |
MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Iringa Mustapher
Msowela amemshitaki mwenyekiti wa chama hicho jimbo la Iringa Mjini,
Frank Nyalusi ambaye jana jeshi la Polisi lilifanikiwa kumtia nguvuni
kabla ya kuachiwa kwa dhamana.
Nyalusi
aliyeshitakiwa katika kituo cha Polisi cha kati cha mjini Iringa jana,
anatuhumiwa kumtusi mwenyekiti wake huyo wa mkoa kupitia mitandao ya
simu; matusi yanayoendelea kuchunguzwa na jeshi hilo.
Nyalusi
amekamatwa kwa tuhuma hiyo ikiwa ni siku chache tu baada ya kudaiwa
kutoa tuhuma za uongo kwa lengo la kujipatia umaarufu dhidi ya
mfanyabiashara maarufu wa mjini Iringa, Salim Asas ambaye pia ni Kamanda
wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa.
Katika
mkutano wa hadhara uliofanywa na Chadema Desemba 21 kwenye uwanja wa
Mwembetogwa mjini Iringa, Nyalusi ambaye pia ni diwani wa kata ya
Mivinjeni alitoa tuhuma zinazowahusisha vijana watatu ambao hata hivyo
hakuwataja majina kwamba walitumwa na Asas kwenda kumuua.
Asas
kwa kupitia kwa wakili wake, Alfred Kingwe amekanusha tuhuma hizo
alizoziita ni za kipuuzi ambazo haziwezi kubebeka hata kwa mzani mdogo
wa kupimia madini.
Ili
kumsafisha mteja wake, Kingwe alisema ndani ya siku 14 toka akabidhiwe
hati ya madai (Demand Note), Nyalusi anatakiwa kuitisha mkutano katika
eneo lile lile alilotolea tuhuma hizo na kuzikanusha vinginevyo
atafikishwa mahakamani.
Akizungumza
na wanahabari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani
Mungi alisema; “Kuhusu tukio la kumtukana mwenyekiti wake wa mkoa,
Nyalusi alikamatwa jana mara baada ya Msowela kuwasilisha malalamiko
yake polisi, akahojiwa na kuachiwa baada ya kukamilisha taratibu za
dhamana.”
Alisema
jeshi la Polisi linaendelea kuchunguza tukio hilo la kijinai na endapo
litathibitika kuwa la kweli, Nyalusi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya
Mivinjeni mjini Iringa atafikishwa mahakamani.
Kuhusu tukio linalomuhusisha na Asas, Kamanda Mungi alisema jeshi la Polisi limefanya mahojiano ya awali na wahusika hao.
“Jambo
hili lipo, tunachunguza; yapo maneno Nyalusi ameyatamka kwenye mkutano
wao wa hadhara kwamba ametishiwa kuuawa, ametumiwa watu watatu kwenda
kumuua wakiwa na visu. Kumtishia mtu ni kosa la jinai na kumtuma mtu
kwenda kumdhuru mtu mwingine ni kosa la jinai, kwahiyo tunachunguza”
alisema.
Alisema
katika mazingira ya uwazi, Polisi inachunguza suala hilo ili kujua
Nyalusi alitishiwa katika mazingira gani; alitishiwa na nani na kwanini
hakwenda kutoa taarifa hiyo Polisi na kufungua kesi ili Polisi iwakamate
wahusika na kulinda maisha yake.
“Lakini
tunajaribu kuangalia kama hakutishiwa na ametamka vile katika mkutano
wa hadhara, lengo lake lilikuwa ni nini na kama anajua madhara yake kwa
jamii iliyosikia taarifa hiyo ni yepi,” alisema.
Alisema
kama itabainika taarifa zilizotolewa na Nyalusi ni za uongo, sheria
itachukua mkondo wake na kama itadhihiri ni za kweli sheria pia
itachukua mkondo wake.
Wakati
Kamanda huyo wa Polisi akitoa taarifa hiyo jana, Nyalusi alikuwa nje ya
ofisi ya kamanda huyo na alipofuatwa na wanahabari kwa ajili ya kutoa
ufafanuzi wa matukio hayo alijibu kwa kifupi akielezea zaidi tukio la
kushitakiwa na mwenyekiti wake wa Chadema mkoa kwamba; “mimi sijamtusi
mtu, anaweza kusema chochote anachoweza kusema yeye na familia yake,
kusema ni hiari yake.
tiko
tiko
Post a Comment