tiko
tiko
Mvua
kubwa zilizonyesha kwa muda mfupi mjini Morogoro zimesababisha mafuriko
baadhi ya barabara kushindwa kupitika na maji kujaa katika baadhi ya
maduka.
Wakazi
wa mji wa Morogoro wakizungumzia mafuriko hayo wamelalamikia
miundombinu mibovu ya barabara kutokana na kuziba kwa mitaro ambapo
wameitaka halmasauri ya mji wa Morogoro kuzibua mitaro hiyo huku baadhi
ya wafanyabiashara wakilalamikia kupata hasara.
Katika
hatua nyingine mto Kikundi uliopo mjini Morogoro umepoteza uelekeo na
kumwaga maji katika soko kuu la mji wa Morogoro na kusababisha maji
kujaa katika maduka huku baadhi ya magari yakiingia kwenye mitaro na
baadhi ya bodaboda zikiwa na abiria zime zama katika maji na kulazimika
kuvutwa.
Kaimu
mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro Phimlemon Magesa akizungumzia
alalamiko hayo ya wananchi hao amesema manispaa wanajitahidi kufanya
usafi lakini tatizo liko kwa wananchi wenyewe kutupa taka kwenye mitaro
na kusabisha mitaro hiyo kuziba na maji kupoteza ueleko na kujaa katika
makazi ya wananchi.
via>> itv.co.tz
tiko
tiko
Post a Comment