tiko
tiko
Mtoto
Abdul Mohamedi (13) ambaye ni mlemavu wa viungo, amelazimika kuishi
darini kwa miezi minne mfululizo kukwepa kudhuriwa na mafuriko kutokana
mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mjini Mtwara.
Bibi wa mtoto huyo anayeishi Mtaa wa
Magomeni Mbezi, Zainabu Lipuga (70), alisema jana kuwa alimpandisha
darini mjukuu wake Novemba mwaka jana baada ya mafuriko yaliyotekea
kipindi hicho.
Kushushwa kwa mtoto huyo kumekuja baada
ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Wananchi (CUF) Manispaa ya Mtwara
Mikindani, kumtembelea Lipunga kwa lengo la kumjengea nyumba imara
kutokana na kuishi katika mazingira hatarishi.
“Nilipoona mvua zinanyesha nikaona bora
nimnusuru mjukuu wangu asisombwe na mafuriko kwa vile sina nguvu za
kuweza kumpandisha na kumteremsha mara kwa mara,” alisema Lipuga na
kuongeza:
“Mjukuu wangu ni mlemavu hawezi hata
kukaa, katika kipindi chote hicho amekuwa akilala tu, najua anateseka
sana hasa ukizingatia umbali wa dari na paa la bati ni karibu sana
wakati wa jua kali anaumia sana ila sina jinsi.”
Alisema baba wa mtoto huyo ambaye ni mwanaye hajulikani alipo na kwamba jukumu la kumlea limeachwa mikononi mwake bila msaada.
Mjumbe wa umoja huo, Mwanahamisi Hamisi
alisema chama chake kimeguswa na hali hiyo, hivyo kimeamua kumuondoa
katika nyumba yenye miundombinu duni.
“Milango ipo wazi kwa wadau wengine
kumsaidia bibi huyu ili aweze kuishi vizuri na mjukuu wake...inatia
huruma yule mtoto anaathirika sana na jua kali kule darini, anahitaji
kusaidiwa,” alisema Mwanahamisi.
Hata hivyo, wakati huo, manispaa hiyo ilikumbwa na mafuriko Januari mwaka huu.
Zaidi ya nyumba 200 zilizingirwa na maji kusababisha hasara kwa wananchi ikiwamo kuharibika mali zao zikiwamo nguo na vyakula.
Katika janga hilo, hakuna mtu aliyeripotiwa kupoteza maisha.
tiko
tiko
Post a Comment