tiko
tiko
Uamuzi
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuahirisha Kura ya Maoni ya Katiba
Inayopendekezwa umewafungulia viongozi wa Ukawa kuishinikiza Serikali
kuiboresha Katiba ya sasa katika maeneo manne ili kuondoa mvutano katika
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Mambo manne yanayodaiwa na Ukawa ambayo
ni ushindi wa urais kuamuliwa kwa asilimia zaidi ya 50, mgombea binafsi
katika nafasi za udiwani, ubunge na urais, tume huru ya uchaguzi na
urais kupingwa mahakamani ni yale yaliyoafikiwa baina ya Rais Jakaya
Kikwete na vyama vya siasa Septemba 8, mwaka jana.
Mwenyekiti mwenza wa umoja huo, James
Mbatia amesema maboresho yaliyofanyika chini ya Kituo cha Demokrasia
Tanzania (TCD) ni ya lazima ili kufanikisha uchaguzi huo kabla ya
kupitishwa kwa Katiba Mpya na kuondoa uwezekano wa vurugu.
Katika kikao hicho, Mbatia alisema
walitiliana saini kuwa iwapo uchaguzi wa mwaka huu utafanyika kwa
kutumia Katiba ya 1977, Bunge lingekutana Novemba mwaka jana kufanya
marekebisho hayo ya 15 ya Katiba na endapo hilo lingeshindikana, basi
lingekutana Februari, jambo ambalo pia halikufanyika.
Utekelezaji wa masuala hayo utawezekana
iwapo Serikali itawasilisha marekebisho hayo bungeni ili yajadiliwe kwa
dharura katika mkutano ujao wa Bajeti wa mwisho wa Bunge la Kumi, kwa
kuwa uwezekano wa kupata Katiba Mpya kabla ya uchaguzi ni kama haupo.
Alipoulizwa iwapo jambo hilo
linawezekana katika Mkutano wa Bajeti, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge,
John Joel alisema: “Ndiyo inawezekana. Serikali inaweza kuwasilisha
jambo hili kwa dharura na litajadiliwa na Kamati ya Uongozi, kama ikiona
linafaa litapelekwa bungeni kujadiliwa.”
Katika hilo Mbatia alisema: “Bado kuna
nafasi ya Bunge kufanya marekebisho. Hili linatakiwa kufanyika kama
ambavyo tulikubaliana na Rais kupitia TCD.”
Alisema ushauri wa TCD kwamba mchakato
wa Kura ya Maoni uahirishwe hadi mwakani umepuuzwa na matokeo yake
yameonekana wazi na kwa msingi huo, suala la kurekebisha maeneo hayo
manne, si la kupuuza hata kidogo.
“Hili lisipofanyika utaibuka mgogoro
mkubwa. Tatizo la Serikali yetu ni kutotaka kutekeleza mambo
yanayoonekana wazi kuwa na mkanganyiko, ndiyo sababu ya kukithiri kwa
migogoro ya wakulima, wafugaji, wafanyakazi na mingine mingi,” alisema
Mbatia.
Dk Slaa akata tamaa
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod
Slaa alisema endapo Serikali itashindwa kutekeleza makubaliano hayo,
vyama vya upinzani havina budi kuingia katika mapambano kwa katiba
hiyohiyo.
“Kama hatumwelewi Rais Kikwete katika
suala hili, basi hatuwezi kumwelewa tena. Sioni juhudi zozote za
Serikali kubadili maeneo haya. Tulikubaliana naye mambo mengi lakini
yote ameshindwa kuyatekeleza, hata hili pia hawezi kulitekeleza,”
alisema Dk Slaa
-mwananchi
tiko
tiko
Post a Comment