tiko
tiko
Jana
Mwanasheria wa askofu huyo Paul Mallya akiambatana na Askofu Gwajima
akiwa kwenye baiskeli ya magurudumu mawili ya kubeba wagonjwa, walifika
katika Kituo Kikuu cha Polisi, jijini Dar es Salaam saa 2.00 asubuhi kwa
ajili ya kuitikia wito wa polisi uliotaka Askofu huyo akahojiwe.
Hata
hivyo, kabla hajamaliza kupandishwa ngazi ya pili kuingia kwenye jengo
la ofisi za kituo hicho, polisi walisema hawawezi kumhoji mpaka afya
yake itakapoimarika.
“Tulifika
(kituo kikuu cha polisi) saa 2.00 asubuhi tukiwa tayari kwa mahojiano.
Askofu alipoanza kupandishwa ngazi akiwa katika wheel chair (baiskeli ya
magurudumu mawili ya kubeba wagonjwa), polisi walipomuona, kabla
hajamaliza kupanda, walitwambia ni vyema akarudi nyumbani mpaka Aprili
9, mwaka huu ndipo wamhoji,” alisema Mallya.
Alisema
kuna mtu aliyetambulika kwa jina la Abubakar Yusufu, mkazi wa Kiluvya,
wilaya ya Kisarawe, mkoa wa Pwani, ndiye amefungua kesi ya jinai polisi
akilalamika kukwazwa na lugha iliyotumiwa na Askofu Gwajima dhidi ya
Askofu Mkuu Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp
Kardinali Pengo.
Askofu Gwajima alifika katika kituo hicho akisindikizwa na msafara wa magari matatu.
Gari
la kwanza lilimbeba Mchungaji Baraka; la pili, aina ya Land Cruiser
alikuwamo Askofu Gwajima na la tatu lilikuwa lake (Mallya).
Tofauti
na ilivyokuwa Jumanne kwa wafuasi wengi wa Askofu Gwajima kufurika
katika kituo hicho na kulilazimisha Jeshi la Polisi liimarishe ulinzi
kwa ajili ya kuwadhibiti, jana hawakuwapo.
Jana Askofu huyo hakuzungumza chochote badala yake Mallya ndiye aliyezungumza kwa kifupi na waandishi.
Mallya alisema Askofu Gwajima amefunguliwa mashtaka ya jinai yanayohusisha kutumia lugha kumkashifu Kardinali Pengo.
Alisema
Yusufu alifungua mashtaka hayo kutokana na picha ya video aliyoiona
kwenye mitandao ya kijamii inayomuonyesha Askofu Gwajima akitumia lugha
ya matusi kumkashifu Askofu Pengo ambayo kisheria ni kosa.
Machi
26, mwaka huu, Jeshi la Polisi Kanda hiyo lilimwamuru Askofu Gwajima
kujisalimilisha polisi kwa tuhuma za kumkashifu Kardinali Pengo.
Baadaye,
Machi 27, Askofu Gwajima alijisalimisha kituo hicho lakini wakati
akihojiwa alizimia akiwa chumba cha mahojiano kisha kukimbizwa katika
Hospitali ya TMJ kwa matibabu.
Jumanne
aliondolewa TMJ na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Oyesterbay na
kuachiwa bila masharti, lakini alielekezwa kuripoti jana katika Kituo
cha Polisi Kati.
tiko
tiko
Post a Comment