Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Charles Hillary wa BBC kurejea Tanzania na kujiunga na Azam TV

tiko tiko
hillary2Ngome ya kituo cha Azam TV inaendelea kuimarishwa, baada ya kuzinduliwa kwa studio kubwa na za kisasa za kituo hicho zilizogharimu zaidi shilingi bilioni 56, inadaiwa kuwa kampuni ya Azam Media itamrejesha nyumbani mtangazaji mkongwe wa BBC, Charles Hillary kwaajili ya kuja kujiunga na Azam TV.


Mchambuzi maarufu wa soka Edo Kumwembe ambaye pia hufanya uchambuzi kwenye kituo hicho, amepost taarfia hiyo kwenye akaunti yake ya Facebook kwa kuandika:
“….Mtangazaji maarufu wa BBC, Charles Hillary, anarudi nyumbani kujiunga na kituo cha Azam TV…..welcome home LEGEND….”
Hillary
Hata hivyo chanzo kingine cha kuaminika cha ndani ya Azam TV kimethibitisha kuwa Hillary anarudi kujiunga na kituo hicho.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top