tiko
tiko
Kijana wa jamii ya wafugaji, Tiga Luchoma (15), ameuawa kwa kushambuliwa na wanyama wakali akiwa machungani.
Katika tukio lingine Flugence Sangana (22), mkazi wa kijiji Kiwurungi, wilayani Songea amejeruhiwa na Chui.
Akizungumza
jana, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Revocatus Malimi,
alilitaja tukio la kuuawa kwa Luchoma kuwa lilitokea juzi majira ya saa 2
asubuhi katika kijiji cha Twendembile ambako wakati akiwa machungani
aliuawa kwa kutafunwa na wanyama wakali ndani ya hifadhi ya Taifa ya
Mbuga ya Selous.
Alisema kuwa masalia ya mwili wake yalikutwa kandokando ya mto Msisima ambako inahofiwa kuwa wanyama hao walimshambulia.
Alisema mpaka sasa wanyama waliomshambulia kijana huyo bado hawajafamika ni wa aina gani na uchunguzi unaendelea.
Alilitaja
tukio jingine kuwa lilitokea juzi majira ya saa 2 asubuhi huko katika
kijiji cha Kiwurungi, ambapo Sangana alijeruhiwa vibaya na chui dume
sehemu mbalimbali za mwili wake.
Alisema Sangana alipatwa na mkasa huo wakati alipokuwa akilinda shamba la mazao lisishambuliwe na nyani.
Alisema
kuwa hata hivyo, chui huyo aliuawa na wananchi waliofika eneo la tukio
baada ya kumsikia Sangana akipiga kelele ya kuomba msaada.
Majeruhi huyo amelazwa katika kituo cha afya cha Muhukuru kwa matibabu zaidi.
Malimi
aliwataka wananchi wanoishi maeneo karibu na mbuga ya wanyama,
kutotembea mmoja mmoja ili kusaidiana wanyama wakali wanapotaka
kuwashambulia.
tiko
tiko
Post a Comment