tiko
tiko
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
Siku
moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza
kumvua uanachama, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kesho atatua
jimboni kwake kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
Uamuzi wa kumfukuza Zitto (pichani)
ulifikiwa juzi ikiwa ni muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali
kesi aliyofungua Januari 2, 2014, dhidi ya Bodi ya Wadhamini na katibu
mkuu wa Chadema, iliyokuwa imeshikilia uanachama wake.
Mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu
ndiye alitangaza kutimuliwa kwa Zitto akisema ni kutokana na kufungua
kesi mahakamani, kinyume na Katiba ya Chadema kipengele cha 8 (a) (x).
Jana, Zitto ambaye ni mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) aliongoza kikao cha kamati
hiyo, kilichojadili taarifa ya Tanesco na baadaye alisisitiza kwamba
hana taarifa rasmi ya uamuzi wa mahakama na atakapoipata atazungumzia
hatima yake.
“Kama mnavyoona mimi naendelea na kazi
na wala sina taarifa rasmi lakini nikipata taarifa rasmi na mimi nitatoa
taarifa rasmi, Ijumaa (kesho) ninakwenda jimboni kuzungumza na
wapigakura wangu ambao niliwaahidi kufanya hivyo kabla ya vikao vya
Bunge kuanza Jumanne ijayo,” alisema Zitto ambaye taarifa zinasema
alikuwa amepapanga kuwaaga wapiga kura na baadaye kutimkia kwenye chama
kipya cha ACT alichokiasisi.
“Muhimu kwangu ni kufanya kazi ya
Watanzania na nitafanya kwa mazingira yoyote yale. Siasa yangu inajikita
katika masuala, siyo watu, ukiandika kuhusu Zitto siyo kwa ajili ya mtu
bali masilahi ya Taifa.
“Nakuzwa, nakomazwa na hii ni changamoto, nitaendelea kufanya kazi zangu hadi nitakapopata taarifa rasmi.”
Mwanasheria wa Zitto, Albert Msando juzi
aliliambia gazeti hili kwamba, anafuatilia uamuzi huo wa mahakama kabla
ya kuona ni hatua gani watazichukua.
ACT wachekelea
Baadhi ya wanachama na viongozi wa Chama
cha ACT mkoani Kigoma wamedai kufurahishwa na uamuzi huo, wakidai kuwa
utakinufaisha chama hicho.
Mkazi wa Mwandiga, Dunia Pemba alisema
Zitto alipaswa kujiondoa ndani ya Chadema pale tu alipovuliwa nyadhifa
zake ili atazame sehemu nyingine yenye demokrasia pana kwa vile chama
hicho kilionyesha hakimhitaji tena.
“Sisi tulitangulia huku ACT na sasa
tunamsubiri kwa hamu, aje kujenga chama hiki ambacho ni tishio kubwa
hapa nchini na bila shaka kitachukua viti vingi vya ubunge katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ndiyo maana kutimuliwa kwa Zitto Kabwe ni
faraja kwetu kwa sababu atapata muda wa kutosha kujenga chama,” alisema
Pemba.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment